‘Funeral’ yawakutanisha Lil Wayne, Birdman

0
681

Miami, Marekani

MWISHONI mwa wiki iliopita rapa Lil Wayne, alikutana na aliyekuwa bosi wake kutoka kundi la YMCMB, Birdman baada ya kuwa kwenye bifu kwa kipindi kirefu.

Lil Wayne alikuwa anaachia albamu yake ya 13, ambayo inajulikana kwa jina la ‘Funeral’ hivyo miongoni mwa wageni ambao waliojitokeza ni pamoja na Birdman. Wawili hao walionekana kuwa na furaha baada ya kukutana jambo ambalo halikutarajiwa na mashabiki wengi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.

Mastaa hao walikuwa na bifu kubwa kwa madai Lil Wayne alikuwa anamdai bosi huyo kiasi cha dola milioni 51, ambazo ni zaidi ya bilioni 117 za Kitanzania, lakini kwa sasa wanaonekana kumaliza tofauti zao.

“Alinipa maisha yake yakawa mikononi mwangu, hivyo tutaendelea kuwa pamoja hadi mwisho wa maisha yetu, hivyo sisi ni YMCMB,” alisema Birdmann.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here