23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Frank Lampard amtaka Drogba Chelsea

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa Derby, Frank Lampard  wakati wowote kuanzia sasa anayetarajia kusaini mkataba wa kuinoa Chelsea, inaelezwa amemtaja mshambuliaji wa zamani klabuni hapo, Didier Drogba kutaka kufanya naye kazi katika benchi lake la ufundi.

Lampard anapewa nafasi  hiyo kubwa ya kuchukua mikoba ya Maurizo Sarri anayetimkia Juventus, baada ya kukiongoza kikosi hicho msimu mmoja pekee na kufanikiwa kukiwezesha kutwaa  ubingwa wa Ligi ya Europa.

 Mchezaji huyo wa zamani klabuni hapo, amebakiza mkataba wa mwaka mmoja pekee na waajiri wake wa sasa Derby, ambao wanahitaji kiasi cha Pauni milioni nne kumuachia.

Hata hivyo, kabla ya kusaini mkataba wa kuinoa  The Blues,  Lampard anahitaji kuwasilina nawatu wake wa benchi la ufundi, miongoni mwao ni mchezaji mwenzake wa zamani, Didier Drogba.

Hatua hiyo inatokana na Drogba kuwa chachu katika  mafanikio ya Chelsea aliyoichezea kwa miaka nane na kufanikiwa kufunga mabao 157,  ambapo uwepo wake utakuwa na msaada mkubwa hasa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Mbali na Drogba, lakini pia Lampard ataongozana na msadizi wake, Jody Morri ambaye pia aliwahi kuichezea Chelsea kuanzia mwaka 1996 hadi 2003, kabla ya kupewa majukumu ya  kuinoa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 16.

Lakini  wengine katika jopo hilo la benchi la ufundi, Lampard amemjumisha  kipa wa zamani wa Manchester City, Shay Given, huku akiwaweka pembeni kina John Terry na msaidizi wa sasa wa Sarri, Gianfrnaco Zola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles