Fisi, mbweha wazagaa mitaani Mwanza

FISINA BENJAMIN MASESE, MWANZA

FISI na mbweha wamekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ilemela, ikielezwa kwamba  wamekuwa wakiingia katika makazi ya watu na kushambulia  mbuzi, matikitimaji na kabeji kwenye mashamba ya wakulima.

Uchunguzi umeonyesha kuwa wanyama hao ambao wameongezeka maradufu katika kipindi hiki cha kiangazi, wamekuwa wakizurura na wakisikika wakitoa milio yao  kati ya  saa 1.00 usiku na saa 12.30  asubuhi   jambo ambalo limeleta hofu kuhusu usalama wao.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, maeneo ambayo wanyama hao wameonekana zaidi ni   Igoma, Kishili, Kakebe, Mahina, Sahwa, Kanindo, Majengo Mapya , Fumagila, Bukaga ambako  mbuzi wa wananchi  wanne wamekwisha kuliwa  pamoja na kuharibiwa mashamba ya matikitimaji na kabeji.

Kuwapo  fisi hao kwa wingi kumeleta hofu nyingine  kwa ndugu wa marehemu waliozikwa na wanaoendelea kuzikwa katika makaburi ya Igoma kwamba yanaweza kufukuliwa na fisi hao ikizingatiwa yamekuwa yakichimbwa kina kifupi baada ya eneo la maziko kujaa.

Katika makaburi ya eneo hilo, baadhi ya marehemu wamekuwa wakizikwa juu ya wengine na Halmashauri ya Jiji la Mwanza tayari imetafuta eneo  la Kanindo,  Majengo Mapya kama mbadala ya makaburi hayo.

Hata hivyo,  bado haijatoa  fidia kwa wamiliki wa ardhi hiyo ili yaanze kutumika.

Gazeti hili  jana lilitembelea mashamba ya wakulima wa matikitimaji  katika bonde la mto Kishili unaopeleka maji yake Ziwa Victoria na kushuhudia uharibifu uliofanywa na wanyama hao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakulima wa mashamba hayo, walisema wanashangazwa na wingi wa fisi na mbweha katika maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here