27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti CCM mbaroni akituhumiwa kuoa mwanafunzi

WANAFUNZINa JUDITH NYANGE, Mwanza

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mtaa wa Sangabuye, John Luhela, anatuhumiwa kukatisha masomo  ya   mwanafunzi  kidato cha pili katika shule ya sekondari Sangabuye, Lucia Daudi,  na kuishi naye kinyumba kwa   mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika mtaa huo,   Luhela alimuoa  mwanafunzi huyo kwa kulipa mahari ya Sh 200,000 na  kusababisha akatishe  masomo yake mwaka jana.

Inasemekana hivi sasa mwanafunzi huyo  ni mjamzito.

Mwandishi alifika nyumbani kwa  Luhela  ambaye alieleza kumfahamu  Lucia  kama mtu wake wa karibu.

Alisema wakati msichana huyo alikuwa amekwenda  nyumbani  kwa mama yake mzazi (mama wa Luhela)  ambako alimwacha baada ya kumaliza msiba wa kaka yake.

Mama yake Luhela naye alisema Lucia alikuwapo hapo lakini aliondoka baada kumaliza kula chakula cha mchana na hakueleza alikoelekea.

Mama wa  Lucia, Agness  Kadirana,  alipoulizwa alisema mwanae aliacha shule mwaka 2013 akidai kuwa shule imemchosha na kwamba alitaka ajifunze ufundi cherehani.

Alisema  mara ya mwisho alimuaga kuwa alikuwa anakwenda Igoma wilayani Nyamagana kwa mdogo wake.

Kuhusu taarifa ya kupokea mahari kwa ajili ya kumuoza mwanae kwa mwenyekiti wa mtaa huo, Agness alikana madai hayo.

Alisema hajawahi kupokea fedha yoyote na hana  lolote  na akasisitiza kuwa hana lolote la kusema kuhusu ujauzito wa mtoto wake kwa sababu mwanae huyo ana baba yake.

Hata hivyo,  Agness, mama mzazi wa Lucia  na mwenyekiti wa mtaa wa Sangabuye, wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Kirumba kwa uchunguzi wa tukio hilo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwalimu Mkuu wa  Shule ya Sekondari Sangabuye, Stephen Mhagama, alikiri  binti huyo  alikuwa mwanafunzi wa shule hiyo.

Mwalimu Mhagama alisema  kwa sasa binti huyo angetakiwa  kuwa kidato cha tatu lakini alianza utoro tangu Juni mwaka jana   baada ya kumaliza  muhula wa kwanza wa masomo.

“Nilijitahidi kufuatilia wanafunzi wote ambao hawahudhurii masomo kupitia  mpango wa kukomesha utoro wa rejareja nikapata taarifa  Lucia amewekwa kinyumba na kiongozi wa serikali ya mtaa wa Sangabuye.  Ndiyo sababu  hakufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili.

“Kwa mujibu wa sheria za  Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, mwanafunzi anapomaliza kidato cha nne  suala la kuolewa linatakiwa kusubiri miaka miwili.

“Akiolewa mara tu  baada ya kumaliza anakuwa  bado ni mwanafunzi, nawaomba wananchi wasitumie hali ngumu ya uchumi wa familia za wanafunzi kuwarubuni,” alisema Mhagama.

Juhudi za mwandishi  kumtafuta mwanafunzi huyo kwa kushirikiana na   polisi wilayani  Ilemela ziligonga mwamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles