24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Abiria wasiofunga mikanda kudhibitiwa

Abiria wasiofunga mikandaNa JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Usalama Barabarani Tanzania limezindua mkakati wa miezi sita kukabiliana na ajali za barabarani.

Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema mkakati huo utahusu  mambo 14 ikiwamo kudhibiti abiria ambao hawafungi mikanda ya usalama wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri.

Akizindua  mkakati huo  Dar es Salaam jana, alisema mkakati huo umeanza kutekelezwa kuanzia jana.

Mkakati huu utakuwa mwiba hususan  kwa mabasi yanayofanya safari zake ndani ya miji maarufu kama ‘daladala’ ambazo nyingi huwa hazina mikanda ya abiria na hata inapokuwa nayo, abiria hawalipi kipaumbele suala la kuitumia, alisema.

Alisema katika   miezi sita itahakikishwa sheria za usalama barabarani na ile ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) zinafanyiwa marekebisho kuongeza makosa ya barabarani yakiwamo yanayowagusa abiria moja kwa moja.

“Katika mkakati huu tutadhibiti abiria ambao hawafungi mikanda ya usalama wanapokuwa katika vyombo vya usafiri, wakati huohuo, tunaendelea kufanya mchakato wa kurekebisha sheria ya usalama barabarani na ile ya Sumatra ili abiria ambaye atafanya kosa aweze kushtakiwa,” alisema Masauni.

Alitaja mambo mengine katika mkakati huo kuwa ni kuanza utaratibu wa  mfumo wa nukta katika leseni za udereva na kudhibiti usafirishaji wa abiria kwa kutumia magari ya muundo wa tairi moja nyuma mfano Noah.

Nyingine ni  kudhibiti madereva walevi na  wazembe, kudhibiti mwendo kasi, uendeshaji wa magari bila sifa, ajali za pikipiki na usafirishaji wa abiria.

Alisema kwa madereva watakaofanya makosa yanayosababisha madhara makubwa hawatapigwa faini tu bali watawekwa mahabusu kwa saa 24 kabla ya kupelekwa mahakamani na kulipa faini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles