32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

Filamu ya nipe changu kuuzwa mtandaoni     

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam  

Filamu ya ‘Nipe Changu’ ya muigizaji Daudi Michael (Duma) kwa sasa itaonekana nchi mbalimbali duniani kupitia zana (app) ya MP Tv.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Duma amesema baada ya filamu hiyo kuoneshwa nchini tu kwa sasa itapatikana kwa kupakua ‘app’ ya MP Tv ambayo wamiliki wake ni Wazambia.

Naye mkuu wa maudhui wa MP Tv, Cassie Kabwita amesema kupitia app hiyo itasaidia kuitangaza na kukuza tasnia ya filamu kiujumla.

“Tumeichukua filamu hii kwa sababu ya stori yake jinsi watu walivocheza inaonesha utamaduni wa kitanzania na tunataka tufanye kazi pamoja na wazalishaji na wasanii wa Tanzania ili tuikomboe sanaa ya filamu,” amesema.

Naye muigizaji wa filamu nchini, Jacob Stephen (JB), ameteuliwa kuwa balozi wa app hiyo ya MP Tv.

JB amesema ni furaha kwa wasanii kupata jukwaa la kuuzia kazi zao mitandaoni.

“Baada ya kuzinduliwa MP Tv sasa naweza kusema hili ni jukwaa zuri kwetu, maana malipo tunayopata kutokana na kazi zetu kuoneshwa katika televisheni ni kidogo tofauti na zinapooneshwa mitandaoni ambapo unalipwa vizuri na hata pesa yako ya uzalishaji inarudi,” amesema JB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles