25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Filamu ya Nipe Changu kuuzwa mtandaoni

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Filamu za Bongo kuuzwa mtandaoni Filamu ya ‘Nipe Changu’ ya muigizaji Daudi Michael (Duma) kwa sasa itaonekana nchi mbalimbali duniani kupitia zana app ya MP Tv.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Duma amesema baada ya filamu hiyo kuoneshwa nchini tu kwa sasa itapatikana kwa kupakua app ya MP Tv ambayo wamiliki wake ni Wazambia.

Naye mkuu wa maudhui wa MP Tv, Cassie Kabwita amesema kupitia ‘app’ hiyo itasaidia kuitangaza na kukuza tasnia ya filamu kiujumla.

“Tumeichukua filamu hii kwa sababu ya stori yake jinsi watu walivocheza inaonesha utamaduni wa kitanzania na tunataka tufanye kazi pamoja na wazalishaji na wasanii wa Tanzania ili tuikomboe sanaa ya filamu,” amesema.

Naye muigizaji wa filamu nchini, Jacob Stephen (JB), ameteuliwa kuwa balozi wa app hiyo ya MP Tv.

JB amesema ni furaha kwa wasanii kupata jukwaa la kuuzia kazi zao mitandaoni.

“Baada ya kuzinduliwa MP Tv sasa naweza kusema hili ni jukwaa zuri kwetu, maana
malipo tunayopata kutokana na kazi zetu kuoneshwa katika televisheni ni kidogo tofauti na zinapooneshwa mitandaoni ambapo unalipwa vizuri na hata pesa yako ya uzalishaji inarudi,” amesema JB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles