25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

FIGISU ZAANZA UCHAGUZI MDOGO

Na WAANDISHI WETU-DAR/TANGA              |        


WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani unaotarajiwa kufanyika Septemba 16 zikianza leo, Mgombea Ubunge wa CCM katika Jinbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava, ametangazwa kupita bila kupingwa kwa madai kuwa mgombea wa Chadema, Amina Saguti, alirudisha fomu baada ya saa 10 jioni jana.

Mkurugezi wa Wilaya ya Korogwe Vijini, Dk. George Nyaronga, aliliambia gazeti hili kuwa kupitishwa kwa Mzava kulitokana na Mgombea wa Chadema kurudisha fomu nje ya muda unaotakiwa katika sheria.

Hata hivyo Chadema kilisema  kuwa mgombea wake alikuwa kwenye ofisi za msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo kuanzia saa 5.00 asubuhi jana.

Katika taarifa yake kilisema  akiwa kwenye ofisi hizo, alizungushwa bila kupewa ushirikiano huku baadhi ya watu wasiojulikana wakijaribu kumnyang’anya fomu zake.

Hali hiyo inajitokeza  zikiwa ni siku chache tangu  ufanyike uchaguzi mwingine mdogo wa ubunge Agosti 12  katika Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma ambakoa CCM ilitangazwa kushinda.

Mgombea Ubunge wa CCM katika Jinbo la Korogwe Vijijini.

Siku hiyo hiyo pia ulifanyika uchaguzi mdogo wa udiwani  katika kata 36 nchini ambao CCM ilinyakua kata zote huku katika kata nyingine 41  wagombea udiwani wake walitangazwa kupita bila kupingwa baada ya wapinzani kuenguliwa katika hatua za awali.

Chadema malalamiko

Akizungumza na MTANZANIA jana,  Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alisema walifika katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi saa 5:38 asubuhi na  walisaini majina yao katika kitabu cha wageni.

“Tulifika tangu saa 5:38 na tulisaini kitabu cha wageni… msimamizi wa uchaguzi akatuambia hapokei fomu mpaka saa 10.00 na kwamba alikuwa ameelekezwa hivyo.

“Tukashangaa!  Ilipofika saa 10:30 jioni mgombea wa CCM akaondoka, sisi tukawa tunajihoji imekuwaje wakati msimamizi hakuwapo ofisini?

“Baadaye saa 11:20 jioni tukamwona mtu anabandika karatasi kuwa mgombea wa CCM amepita bila kupingwa.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles