30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEPIGWA RISASI NA ASKARI MAHAKAMANI DAR ATELEKEZWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro.

Na ZAKIA NDULUTE (UoI)-DAR ES SALAAM


MKAZI wa Mabibo Jeshini, Dar es Salaam, Gabriel Msuya (19), ambaye alijeruhiwa kwa risasi na askari wa Jeshi la Magereza wiki iliyopita, amelalamikia kutelekezwa na mamlaka zilizomjeruhi, huku ndugu zake wakihangaika kumpatia matibabu.

Msuya alipigwa risasi Agosti 16 akiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, alipokwenda kusikiliza kesi yake.

Katika tukio hilo, Msuya alipigwa risasi moja na kujeruhiwa kiunoni na alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala kutibiwa kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Mloganzila iliyopo Kibamba wilayani Ubungo.

Jana, baba mzazi wa kijana huyo, Cornel Msuya, aliliambia gazeti hili kwamba mwanawe bado amelazwa Mloganzila, lakini akalalamikia kuwa hapewi ushirikiano wowote katika matibabu.

“Tangu mgonjwa alipopelekwa Hospitali ya Mwananyamala na kuhamishiwa Hospitali ya Mloganzila, hatujapata ushirikiano wowote wala kuulizwa maendeleo ya hali yake.

“Gharama zote za matibabu nimekuwa nikilipa mimi na hali ya mgonjwa si nzuri. Bado fahamu hazijarudi vizuri na hana uwezo wa kukaa na kula chakula mwenyewe,” alisema.

Mzazi huyo aliziomba mamlaka zinazohusika kumsaidia gharama kwa sababu mwanawe anahitaji matibabu ya haraka aweze kupona. 

POLISI WAENDELEA KUCHUNGUZA

MTANZANIA lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro, ambaye alisema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

“Unataka kujua siri za uchunguzi tunaofanya… uchunguzi unaendelea vizuri na pindi tutakapokamilisha tutatoa taarifa rasmi,” alisema Kamanda Muliro.

Wiki iliyopita, alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa katika mazingira yaliyopo, askari waliokuwepo eneo la tukio ni wa Jeshi la Magereza, ambao hata hivyo hawajakamatwa kwa hiyo taratibu zote za kisheria zitafuatwa uchunguzi utakapokamilika. 

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles