24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

FCS washeherekea ‘Giving Tuesday’

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga

Na Mwandishi Wetu,

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society, limeadhimisha siku ya ‘Jumanne ya Kutoa’ maarufu ‘Giving Tuesday’ kwa kutoa misaada mbalimbali katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam.

Shughuli hiyo inaadhimishwa kila Jumanne ya mwisho ya mwezi Novemba duniani kote na kwa hapa Tanzania ni mara ya kwanza kuadhimishwa.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga, alisema shirika kwa kutambua umuhimu wa mashirika, makampuni na watu binafsi katika jamii, limeamua kuleta utamaduni huo nchini na hiyo inapaswa kuwa ni moja ya shughuli zinazotakiwa kufanywa na kila shirika walau mara moja katika mwaka.

Mkurugenzi huyo alisema wafanyakazi wa shirika hilo waliamua kuchangia  shughuli hiyo kwa asilimia moja ya mishahara yao kwa miezi sita na kampeni nzima imesaidia kukarabati choo kimoja  kinachotumiwa na wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza katika shughuli hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala kutoka katika Wizara ya Elimu, Pancras Steven, alishukuru kwa mchango huo wa FCS.

Steven alisema  shirika hilo limeonyesha   liko makini na kwamba linajali maendeleo ya kila watu na hasa walio na uhitaji zaidi.

“Kazi hii mliyofanya ni kubwa, nawapongeza, nitumie nafasi hii kuwaomba Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia katika majukumu ya maendeleo katika jamii.

“Kwa kufanya hivi mnasaidia sana kuhamasisha jamii nasi kama Serikali tunaungana nanyi,” alisema.

Mwalimu Mkuu wa Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana, aliishukuru FCS kwa kuichagua shule hiyo.

Alisema shule hiyo ina uhitaji mkubwa ikizngatiwa wanafunzi wanaosoma katika shule yake ni tofauti na  wanaosoma katika shule nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles