23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

FAO YATOA MILIONI 280/- MCHAKATO SERA YA MISITU

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


SERIKALI ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), wamesaini makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali  Gaudence Milanzi, alisema  mpango huo utagharimu kiasi cha Sh milioni 280 ambazo zimetolewa na FAO kufanya utafiti wa kuongezea takwimu ambazo zitaboresha Sera ya Misitu ya Taifa  ili iweze kufikia hadhi ya kimataifa.

Alisema hatua hiyo imekuja kutokana na Sera ya Misitu ya Taifa ya mwaka 1998 inayotumika hivi sasa kupitwa na wakati yakiwemo mabadiliko ya kiuchumi, kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

“Sera ya Taifa ya Misitu ilishafanyiwa mapitio kuanzia mwaka 2009, lakini kutokana na sera hii kukaa kwa muda wa takribani miaka 9 hadi hivi sasa tumegundua kuwa baadhi ya wadau wengi hawakupata nafasi ya kutoa mawazo yao. Hata wale waliotoa mawazo yao mengi yameshapitwa na wakati,” alisema Milanzi.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero, alisema mradi huo utasaidia wananchi wengi kushiriki na kutoa mawazo mengi kuhusiana na Sera ya Misitu ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo watumishi kuweza kukusanya taarifa nyingi ili ziwezeshe kuboresha sera kupitia tafiti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles