23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MTO NILE KESHO

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


NCHI wanachama wa Umoja wa Ushirikiano wa Mto Nile (NBI), kesho zinaadhimisha mwaka wa 18 tangu kuanzishwa umoja huo mwaka 1999.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge, alisema maadhimisho hayo yanayoitwa Siku ya Nile yatafanyika jijini kwa matembezi na shughuli nyingine.

Alisema matembezi hayo yataongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na yataanzia Mnazi Mmoja hadi Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

 “Lengo la Siku ya Nile ni kukuza welewa kwa watu wote kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zote 10 wanachama, masuala yanayotekelezwa na faida inayopatikana kutokana na matumizi bora ya rasilimali za Bonde la Mto Nile,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, Lwenge alisema hivi sasa maeneo ya vijijini wanapata maji kwa wastani wa asilimia 72 huku mijini wakipata kwa asilimia 86.

Alisema katika mwaka huu wa fedha itatengwa bajeti zaidi kumaliza suala la maji nchi nzima.

“Hivi sasa tunapeleka maji vijijini kwa wastani wa asilimia 72, si vyote lakini kuna vijiji vingine vinavyopata kwa asilimia 30. Pia mijini wanapata kwa asilimia 86 hivi sasa,” alisema Lwenge.

Maadhimisho hayo hufanyika kila Februari 22, kila mwaka katika nchi mojawapo mwanachama.

Nchi 10 wanachama wa NBI ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda,   Burundi, Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Misri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles