31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

“Fanyeni kazi usiku na mchana wananchi wapate maji”Aweso

Na Amina Omary, Tanga

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Maji, Joyce Msiru na timu ya Wataalamu kutoka Wizarani kubaki Wilaya ya Handeni kuhakikisha wanakuja na mkakati mahsusi wa kutatua kero ya upatikanaji wa huduma ya maji wilayani humo, mkoani Tanga.

Aweso ametoa agizo hilo leo Ijumaa Agosti 27, hiyo alipotembelea vyanzo na miradi ya maji vilivyopo wilayani humo. Handeni.

“Lakini pia natoa siku 30 kwa watendaji wa Sekta ya Maji wilaya ya Handeni, kuhakikisha mnafanya kazi usiku na mchana na kuboresha uendeshaji ili wananchi wapate maji.

“Katika mwaka wa Fedha 2021/22, Serikali imetenga zaidi ya Sh bilioni 21 katika Mkoa wa Tanga ili kutekeleza miradi ya maji vijijini ikiwemo wilaya ya Handeni, hivyo ni haki yenu kupata maji,” amesema Aweso.

Katika hatua nyingine, Aweso amefanya mabadiliko ya kiutendaji na kuahidi kuleta nguvu mpya itakayoboresha eneo la uendeshaji na usimamizi ila kuleta mabadiliko Mji wa Handeni na viunga vyake.

Pamoja na mambo mengine, Aweso amesema Wizara ya Maji iko katika hatua za mwisho katika kukamilisha zabuni ya utekelezaji wa miradi ya maji kwenye miji 28 nchini pia utekelezaji wa mradi wa HTM utakamilika na kumaliza kabisa changamoto ya maji wilayani Handeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles