24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Liver v Chelsea balaa zito EPL

ACHANA na vita ya pale Etihad kati ya wenyeji Manchester City na Arsenal. Mikikimikiki ya Ligi Kuu England (EPL) wikiendi hii itapambwa na dakika 90 za moto kati ya Liverpool na Chelsea.

Kwa upande mwingine wa mchezo huo, unaweza kusema hii ni vita ya makocha wawili wenye mafanikio makubwa tangu walipotua EPL, Pep Guardiola na Jurgen Klopp.

Ifahamike kuwa Liverpool dhidi ya Chelsea unakwenda kuwa mchezo wa tatu kwa kila timu tangu msimu huu wa EPL ulipoanza kutimua vumbi wiki chache zilizopita.

Hivyo basi, makala fupi haya yanakuibulia rekodi mbalimbali zilizoko kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa kandanda la England.

01. Kila timu imeshinda mechi zake mbili za kwanza na hakuna iliyoruhusu nyavu zake kutikiswa. Liverpool imeziua Norwich City (3-0) na Burnley (2-0), huku Chelsea ikizifunga Crystal Palace (3-0) na Arsenal (2-0).

02. Liverpool wamefungwa mechi mbili tu kati ya 13 za EPL walizokutana na Chelsea hivi karibuni. Takwimu zinaonesha kuwa Liverpool imeshinda sita na kutoa sare moja katika mechi 11 zilizobaki.

03. Ukiacha Man United iliyoshinda mechi nyingi (12) za EPL katika Uwanja wa Anfield, Chelsea wanafuata wakiwa wameondoka na ushindi mara saba, ikiwamo mechi ya kwanza ya msimu uliopita.

04. Tangu msimu huu uanze, Liverpool ndiyo timu iliyopiga mashuti mengi (46), wakati Chelsea ndiyo timu iliyoruhusu wapinzani kupiga mashuti machache zaidi (10).

05. Endapo itashinda, basi itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 kuiona Chelsea ikishinda mechi tatu mfululizo za mwanzoni mwa msimu bila kuruhusu bao.

06. Mechi ya mwisho kuzikutanisha timu hizi ni ile ya Machi, mwaka huu, na dakika 90 zake zilimalizika kwa Chelsea kushinda bao 1-0, mfungaji akiwa ni Mason Mount.

07. Pigo kwa Liverpool ni kwamba huenda ikamkosa kiungo wake mzoefu, James Milner. Chelsea hawatakuwa na huduma ya Ruben Loftus-Cheek na Christian Pulisic kwa kuwa wana Corona.

08. Vikosi – Liverpool: Alisson, Robertson, Van Dijk, Matip, Alexander-Arnold, Fabinho, Keita, Henderson, Mane, Jota na Salah.

Chelsea: Mendy, Christensen, Rudiger, Azpilicueta, Jorginho, Kante, Alonso, James, Mount, Havertz na Lukaku.

09. Tangu kocha Thomas Tuchel alipoanza kazi, Chelsea imeruhusu mabao 17 tu katika mechi 33. Hiyo inamaanisha washambuliaji wa Man City wanapaswa kuja na nguvu ya kutosha.

10. Liverpool imeziona nyavu za timu pinzani katika mechi zote 12 za Ligi Kuu ilizocheza hivi karibuni (mbili za msimu huu, 10 za mwishoni mwa msimu uliopita).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles