26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Ethiopia waongoza kasi ya wahamiaji haramu

Na Oliver Oswald, Mtanzania Digital

Raia wa Ethiopia wametajwa kuongoza kwa idadi kubwa ya wahamiaji haramu nchini wanaoingia kwa njia zisizo  halali (njia za panya).

Akizungumza na Mtanzania Digital, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle amesema baadhi ya raia hao huingia nchini kupata urahisi wa kuendelea na safari zao kwenda mataifa mbalimbal duniani.

Mselle amesema sababu kubwa inayochangia waethiopia wengi kuingia nchini, moja wapo ni kutafuta urahisi wa njia za kufika katika nchi zilizo endelea.

“Kutokana na kukosa kibali halali cha kuingia nchini wahamiaji haramu wengi hulazimika kutumia njia zisizo ruhusiwa kuweka makazi ya kujificha kuendelea na safari zao za magendo.

“Mfano baadhi ya wahamiaji haramu wanaoingia nchini kuweka makazi ,wengi wao hutoka nchi zilizo tuzunguka ikiwemo burundi,” amesema Mselle.

Pamoja na hayo Mselle amezitaja njia zinazo tumika kusafirisha wahamiaji hao kuwa ni malori yanayopeleka bidhaa nje ya nchi na pikipiki.

Amesema baadhi ya madereva wa malori hupatwa tamaa ya fedha za haraka na hivyo hushawishika kufanya uhalifu huo kwa kuwasafarisha na kuwavusha kwenye mipaka kinyume cha sheria.

“Madereva hao wanapogundua mbele kutakuwa na vikwazo cha kushindwa kuwavusha, baadhi hutelekeza magari yao au hulazimika kwenda kuwaombea hifadhi kwa wakazi walio karibu na maeneo hayo.

“Pindi raia wema wanapoona watu wasio waelewa katika vijiji vyao wakiwemo wahamiaji haramu hujakutoa taarifa katika vituo vyetu vilivyomo katika kata na wilaya,” amesema.

Mselle alizataja changamoto wanazo kutana nazo pindi wanapoenda kufanya doria ya kuwa kamata wahamiaji haramu walio jificha katika vijiji na maeneo mbali mbali nchini, kuwa ni pamoja na kushindwa kufika maeneo hatarishi wanayo kimbili.

Alisema miongoni mwa njia hatarishi zinazotumiwa na wahamiaji haramu hao ni pamoja na kwenye mbuga za wanyama, baharini, kwenye vichaka ambapo magari yao ya doria hushindwa kupita katika njia hizo.

“Tunapokuwa  tuna wafatilia wahamiaji hao kwa lengo la kuwakamata hutumia pikipiki kukimbilia vichakani na kwenye njia ambazo magari yetu haya wezi kupita.

“Mbali ya changamoto hizo huwa tunawakamata kwa kudhibiti njia zilizopo mipakani ambapo taarifa zao huwa zimeshafika,” amesema.

Amesema wengi wa wahamiaji haramu hao wanao ingia nchini na kukamatwa huanzia miaka 18 na kuendelea ambapo hutozowa faini ya Sh milioni 20 au kutumikimia kifungo cha miaka ishirini jela.

Alieleza kwamba katika kuhakikisha wanapambana na wahamiaji haramu nchini hufanya doria kwenye hotel mbali mbali na mitaa ili kuwabaini watu hao.

“Pia huwa tunatoa elimu katika ngazi ya kata na wilaya kwa kuzungumza na viongozi wa kijiji au watendaji wa serkali za mtaa ili kuweza kufikisha elimu hii kwa  wananchi kujua jinsi gani ya kutoa taarifa za wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila kibali,”amesema Mselle.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles