23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

50 Cent, Chid Benz walinivutia kufanya HIP Hop- XMG

Na Oliver Oswald Mtanzania Digital

“Cha kwanza nilikuwa naupenda Muziki , kwahiyo nilikuwa natamani kufanya aina fulani ya muziki kwa utunzi tofauti lakini wenye miondoko ya kufoka yaani “Hip Hop”…..Hivi ndivyo anavyo anza kutuelezea , Msanii wa Muziki wa kufoka Steve Bella Rushatsi au kwa jina lingine XMG kama anavyo julikana kwenye kazi yake ya muziki wa kizazi kipya.

Xmg ambalo kirefu chake ni ‘Xcilla Moon God’ likiwa na maana ya ‘Mmea usiokauka’ anasema alianza rasmi kujihusisha na uimbaji Mwaka 2009 akiwa anaimba mwenyewe bila kurikodi , lakini ilipofika Mwaka 2012 alifanikiwa kurikodi wimbo wake wa kwanza uliokuwa ukiitwa “Ndo kwanza naanza”.

50 Cent

Anaeleza kwamba tangu alipoanza kurikodi wimbo wa kwanza Mwaka 2012 hadi sasa anazaidi ya nyimbo 100 zilizokuwa tayali studio na kati ya hizo amesha achia nyimbo nne ambazo ni Snitch aliyo mshirikisha mdogo wake Amani Bella Rushatsi (‘Starzan’ kama anavyo julikana kwenye Sanaa).

Nyimbo nyingine ni love in a cup na last king stand ambapo kati ya hizo wimbo wa Snitch pekee ndiyo uliofanyiwa video akiwa na familia yake.

“Kwa sasa nafanya shughuli zangu za muziki mwenyewe kama ‘Solo Artist’ ila baadae nina mpango wa kuanzisha ‘Xmg Gang’ kama kikundi cha wasanii wangu yaani ‘Lebo’.

“Pia walionivutia zaidi mimi kupenda Sanaa ya kuimba muziki wa kufoka ni Rapa mkongwe kutoka nchini Marekani ambao ni ’50 Cent, Nelly, 2Chains, Future na 8Ball.

“Kwa upande wa hapa nyumbani Tanzania wasanii wa Hip Hop walio nishawishi kupenda kuimba aina hii ya muziki ni pamoja na Chid Benz na Godzilla,” anasema.

Siku zote kwenye mapambano hapakosi changamoto na Xmg anaeleza kuwa miongoni mwa changamoto alizowahi kukabiliana nazo katika harakati zake za uimbaji ni pamoja na Baba yake Mzazi Mzee Rushatsi, kumwambia kuwa aachane na kazi hiyo kwani haina faida pia ni uhuni.

Anasema kutokana na kauli hiyo kutoka baba yake mzazi , ilisababisha akose sapoti kutoka kwenye jamii inayo mzunguka ikiwemo ndugu na jamaa wa karibu.

“Mwanzo Baba alinikatisha tamaa lakini sikugeuka nyuma kwani nilikuwa najua nini nacho kifanya na kwa sababu nilikuwa nakipenda ilibidi waniache na mpaka sasa hata mzee mwenyewe ameanza kunielewa.

“Lakini changamoto kubwa inayo tukabili wasanii wengi tunaoimba hip hop ni kwa Masponsa kutokuupa sapoti kwa kudhana ya kwamba aina hii ya muziki ni wa kigeni wakati si kweli,” anasema.

Anasema, wafanyabiashara wengi wa kazi za Sanaa hapa nchini , wanaidharau hip hop kwa kusema kwamba haina mashabiki wengi na ni muziki mgumu kuuelewa na hata kufanikiwa kibiasharaikilinanishwa na aina nyingine ya muziki kama Afropop, Zuku na Amapiano.

Xmg anabainisha kwamba muziki wa hip hop unapendwa na unamashabiki wa kutosha ila Masponsa wengi nchini huangalia ni muziki upi unaotamba kwa kipindi husika ikilinganishwa na  nchi za wenzetu ambapo aina zote za muziki zinatoka kibiashara.

Sambamba na changamoto hizo za kibiashara pia anasema kutokana na kuwa na ajira sehemu nyingine hukosa muda wa kutosha kwa ajili ya kuzunguka katika vyombo vya habari ili kutangaza kazi zake hali inayo sababisha kushindwa kuwafikia wasikilizaji wengi kwa muda unaotakiwa.

“Mbali na shughuli zangu za kuimba lakini pia mimi ni mwajiriwa kwahiyo mara nyingi huwa nashindwa kuutumia muda wangu sahihi niliojipangia kwa ajili ya kufanya muziki.

“Hali hiyo ilinilazimu kufungua Studio nyumbani kwangu kwahiyo hata nikichelewa kurudi basi shughuli zangu za kurikodi huwa nazifanyai kwangu na mke wangu ndo huwa Produsa,” anasema Xmg.

Anasema ushirikiano mkubwa anaoupata kwa familia yake akiwemo mkewe na watoto wake wawili humuongezea hali ya kupambana Zaidi kufikia mafanikio waliyonayo wasanii wakubwa wa hip hop nchini na nje ya nchi.

Xmg anasema bado hajapata mafanikio yoyote kupitia kazi yake ya Sanaa ila ana Imani ipo siku moja ndoto yake itafanikiwa na atajulikana kama wanavyo julikana wasanii wengine kwa sasa.

Anaelezea pia moja ya ndoto yake kubwa katika Sanaa anayoifanya ni kufanya kazi na baadhi ya wasanii wakubwa nchini akiwemo Chid Benz na Mr Blue ambao anawakubali katika kazi zao kwa muda mrefu.

“Hapo baadae kama ntapata fursa ninatamani siku moja kuwashirikisha Chid Benz na Mr Blue katika baadhi ya nyimbo zangu kwani napenda aina yao ya uimbaji wanavyo tiririka na mashairi”

“Ili haya yote yatimie nawaomba masosponsa wanao husika na masuala ya muziki hapa nchini wajitahidi kutusapi hata kama ni kwa uchache ili kazi zetu ziweze kufiuka mbali kama wasanii wa aina nyingine ya muziki na matokeo mazuri yataonekana”

“Pa vyombo vya habari nchini ikiwemo Televisheni , Redio, Magazeti pamoja na mitandao ya kijamii vitupe ushirikiano wasanii wote na sio kubagua maarufu na wachanga kwani haileti usawa maana wote tunafanya kazi aina moja,” anasema.

Xmg anaelezea kwamba kwa sasa anampango wa kuendelea kufanya video ya nyimbo alizo zirikodi ili aanze rasmi kuzitangaza kazi zake katika vyombo vya habari nchini.

Anasema kutokana na kukosa msimamizi wa kazi zake kwa sasa ameamua kujisimamia mwenyewe na kupambania mafanikio yake mwenyewe hadi atakapo anzisha rasmi Lebo yake ‘Xmg Gang’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles