23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

CCM yampa siku 14 Kairuki kukipa vifaa kituo cha afya Mikese

Na Ashura Kazinja, Mikese

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimempa siku 14 Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki kuhakikisha kituo cha Afya Mikese kinapata vifaa tiba katika wodi ya mama na mtoto na kuweza kufanya kazi sababu licha ya majengo kukamilika kimeshindwa kutumika kwa miaka mitatu Sasa.

Katibu Mkuu CCM Taifa, Daniel Chongolo ameyasema hayo jana wakati akiwa kwenye ziara ya siku 9 mkoani hapa ambapo alisema haiwezekani Jengo lililogharamia mabilioni ya shilingi likashindwa kufanya kazi hasa kwenye Sekta ya upasuaji huku wagonjwa wakikimbilia kata jirani kupata huduma wakati kituo chao kipo.

Alisema chama hakiwezi kudumu kama mambo ya maendeleo kwa wananchi hayaendi na ndio maana Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutatua changamoto za kijamii ikiwemo elimu, Afya na maji.

Alisema Serikali imeshapeleka zaidi ya Sh bilioni 1 katika ujenzi wa kituo hicho huku ikiiagiza Halmashauri kuongeza fedha ambapo zilifikia jumla ya Sh bilioni 2.5 ambazo zinaweza kukamilisha ujenzi pamoja na kupatikana kwa vifaa.

“Serikali imeshaleta vifaa karibu asilimia 80 bado 20 tu, Sasa fedha zilizopo kwa nini msizitumie kukamilisha palipobaki na wananchi wapate huduma, sababu mnasema kituo kina miaka mitatu tangu kijengwe hakijaanza kutumika, bado ni shida kwa wananchi, tutatue hili,” alisema Chongolo.

Hivyo, Chongolo aliwaagiza madaktari 8 waliopaswa kuwepo kituo hicho cha Afya kuendelea kusubiri kutoa huduma kituoni hapo kwa sababu anafuatilia suala hilo na kuhakikisha kituo hicho kinaanza kazi mwishoni mwa.mwezi Machi mwaka huu.

Pia, Chongolo alikemea tabia ya wafugaji na wakulima kuwa na migogoro isiyo na tija bali aliwataka kuwa na umoja utakaowaweka sawa katika shughuli zao za kuwaleta maendeleo.

Hivyo alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Rebecca Nsemwa kuhakikisha anakaa kikao na wananchi hao ili kutatua changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo mara nyingi imekuwa ikisababishwa na baadhi ya viongozi ambao huwapa kiburi.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Robert Manyerere aliiomba Serikali kuwasaidia Kiasi cha sh mil 200 ili wanunue vifaa mbalimbali vinavyohitajika kituoni hapo na kituo hicho kuanza kufanya kazi kwa kutoa huduma zote.

Akisoma taarifa ya kituo hicho Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Mikese, Piencia Mushi alisema kituo hicho kilikamilika tangu mwaka 2021 ambapo kinaendelea kutoa huduma kwa wananchi na kushindwa kuhudumia katika Sekta ya upasuaji kutokana na kukosa Vifaa.

Naye Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Mashariki, Hamisi Taletale aliishikuru Serikali kwa jitihada walizozionesha kwenye Jimbo hilo licha ya kukabiliwa na changamoto ya kutokamilika kituo cha Afya Mikese na kukosekana kwa kituo cha Afya na uchache wa ardhi kulingana na watu waliopo na migogoro ya mipaka Ngerengere.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles