22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Emery afurahia matunda ya mwisho ya Ramsey

LONDON, ENGLAND

BAADA ya kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey, kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Napoli kwenye michuano ya Europa, kocha wa timu hiyo, Unai Emery, amedai wanafaidi matunda ya mwisho ya mchezaji huyo.

Mchezo huo ambao umepigwa juzi kwenye Uwanja wa Emirates, ulikuwa wa robo fainali ya kwanza ya michuano hiyo kabla ya marudiano Aprili 18.

Ramsey raia wa nchini Wales, amekuwa ndani ya kikosi cha Arsenal tangu mwaka 2008, lakini inasemekana kuwa tayari mchezaji huyo amemalizana na uongozi wa klabu ya Juventus kwa ajili ya kutaka kujiunga na kikosi hicho baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari amewaaga wachezaji wenzake mara baada ya kufikia makubaliano na Juventus.

Hata hivyo, mbali na kusaini mkataba na timu hiyo ambayo inafanya vizuri nchini Italia, mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Arsenal huku akiamua kujitoa kwa kiasi kikubwa ili kuacha kumbukumbu kwa mashabiki na historia ya timu.

Mchezaji huyo alipachika bao katika dakika ya 14, kabla ya beki wa timu ya Napoli, Kalidou Koulibaly, kujifunga wakati anawania kuokoa mpira.

“Kwa kiwango ambacho anakionesha kwa sasa mchezaji huyo ni wazi kuna kitu muhimu anataka kutuachia, kwa sababu bado anaipigania timu bila ya kujali kwamba tayari amesaini mkataba wa kuitumikia Juventus msimu ujao.

“Ukweli ni kwamba, anatupatia kile ambacho tunakihitaji, nataka kufurahia kipindi hiki nikiwa na mchezaji huyo, nataka kufanya kitu muhimu na mchezaji huyo kwa kuwa anachokifikiria kwa sasa ni Arsenal, tunafaidi matunda yake kwa mara ya mwisho,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo, kocha huyo anaamini bado ana nafasi ya kwenda kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Napoli ambapo Arsenal watakuwa ugenini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles