24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Edward Lowassa afariki dunia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia leo Februari 10,2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango ametangaza taarifa za kifo cha Lowassa muda huu akiwa mubashara kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) wilayani Munduli mkoani Arusha.

Na katika ukurasa rasmi wa Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameandika ujumbe ufuatao 

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa. Mheshimiwa Lowassa ameitumikia nchi yetu katika nafasi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 35, akianzia ushiriki wake katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge, Waziri katika wizara mbalimbali na Waziri Mkuu.Tumempoteza kiongozi mahiri, aliyejituma na kujitoa kwa nchi yetu. Natoa pole kwa mjane, Mama Regina Lowassa, watoto (Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa na wadogo zako), ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mzito.

Katika mawasiliano yangu na familia, nimewaeleza kuwa kama taifa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu, na kamwe wasiache kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutafakari neno lake, hasa Kitabu cha Ayubu 1:21.” Mwisho wa kunukuu

Taarifa zaidi zitakufikia kadri zitakavyotufikia.

Mungu ailaze Roho yake Mahala Pema Peponi, Ameen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles