27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

DRAKE BADO ANAMUOTA RIHANNA

LAS VEGAS, MAREKANI

UHUSIANO wao wa kimapenzi ulivunjika mwaka jana, lakini bado jina la mrembo Rihanna limeonekana kubaki kichwani kwa Drake mpaka leo hii.

Ripoti zimedai kwamba, Drake amekuwa akimtumia meseji Rihanna tangu zilipoibuka taarifa za mwanadada huyo kutoka na bilionea wa Saudi Arabia, Hassan Jameel. “Drake ‘anammis’,” kilisema chanzo kimoja kuuambia mtandao wa TMZ, ambao ni maarufu kwa habari za uhakika za wasanii.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, tayari Rihanna ameshajua kwamba Drake anamuonea wivu.

Mwezi uliopita, japo hazikuthibitishwa, kulikuwa na taarifa zilizodai Drake amekuwa akimshawishi Rihanna kutemana na tajiri Jameel, ili wafufue mapenzi yao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles