23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

JAY Z AANIKA SIRI YA MAPACHA WAKE

LOS ANGELES, Marekani

BAADA ya ukimya wa muda mrefu, rapa Jay-Z amefichua siri ya majina ya mapacha aliojifungua mkewe, Beyonce, Rumi na Sir.

Jay-Z alisema jina la Rumi walilompa mtoto wao wa kike ni la mwandishi wa mashairi wa zamani, ambaye wamekuwa wakizipenda kazi zake.

“Rumi ni mwanamashairi tunayempenda, tukaona tumpe mtoto wa kike,” alisema rapa huyo.

“Rumi alikuwapo katika karne ya 13, ni mwanamashairi wa kiume, muumini na msomi wa Kiislamu na licha ya kuzaliwa miaka 800 iliyopita, tungo zake za mapenzi bado zinauzika sana Marekani,  kwa mujibu wa BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza).

Aidha, kuhusu jina la Sir, alilompa mtoto wa kiume, alisema halina maana yoyote zaidi ya lilivyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles