30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

JUX AENDELEA KUMNG’ANG’ANIA V MONEY

Na JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM

LICHA ya ‘couple’ ya mastaa Vanessa Mdee ‘V Money’ na  Juma Mussa ‘Juma Jux’ kufikia mwisho, Jux ameibuka na kusisitiza kuwa, atendelea kuwa karibu na mwanadada huyo kwa kuwa bado anampenda.

Jux alisema ni kweli wameachana, baada ya kushindwa kufikia mwafaka wa tatizo lao, lakini wataendelea kuwa karibu kutokana na ustaa wao na urafiki.

Akizungumza na MTANZANIA, Jux alisema wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa miaka minne, lakini kila mmoja ameridhia uhusiano wao kufikia ukingoni na sasa wataendelea kuwa karibu katika kazi zao.

“Nimekuwa katika mahusiano na Vanessa kwa miaka minne, kabla ya hapo tulikuwa marafiki wa muda mrefu, tumeshindwa kufikia mwafaka na ndiyo maana kila mmoja ameridhika kuachana kwetu, ingawa watu watambue kuwa wataendelea kutuona pamoja kwa sababu sisi ni watu maarufu na tutaendelea kufanya kazi pamoja,” alisema Jux.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles