28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

SHAHIDI WA PILI KESI YA AGNES MASOGANGE AFUNGUKA

Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM
SHAHIDI wa pili katika kesi inayomkabili msanii, Agnes Gerald maarufu Masogange, amedai mahakamani alimpeleka mshtakiwa huyo kwa mkemia na mkojo wake ulikuwa na rangi ya njano iliyopauka.

Shahidi huyo ambaye ni Ofisa Mpelelezi, Judith alidai hayo baada ya kuhojiwa na Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Alidai alimpeleka Agnes katika ofisi hizo, Februari 15, mwaka hui, kutokana na kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya au kusafirisha.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constatine Kakula, kutoa ushahidi, Judith alidai siku hiyo alikuwepo ofisini akifanya kazi za kawaida, ambapo naibu mkuu wa upelelezi wa kanda hiyo, Ramadhani Kingai, alimwelekeza kumchukua Agnes na kumpeleka kwa mkemia.

“Nilimchukua Agnes nikiwa nimeambatana na ofisa wa polisi Sospether hadi kwa mkemia mkuu ambapo tulifika saa saba mchana.

“Tulipofika Sospether alienda kujaza fomu huku mimi nikiwa na mtuhumiwa tulienda mapokezi kwa taratibu nyingine.

“Nikiwa mapokezi nilikabidhiwa chupa ndogo ya plastiki iliyokuwa na namba 006/2017 na kuelekezwa nimpeleke kwenye choo maalumu kwa ajili ya kutoa sampuli ya mkojo,” alidai.

Shahidi huyo alidai aliondoka na mtuhumiwa huyo hadi chooni ambapo aliingia huku yeye akiwa nje na baada ya hapo alitoka na sampuli ya mkojo ambayo alienda kumkabidhi Sospeter. Shahidi huyo alimtambua Agnes mahakamani hapo kwamba ndiye aliyempeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali.

Akihojiwa maswali na wakili wa utetezi, Reuben Simwanza, shahidi huyo alidai alikabidhiwa mtuhumiwa huyo kumpeleka kwa mkemia na kwamba alitoa mkojo ambao ulikuwa na rangi ya njano iliyopauka. Shauri hilo limepangwa kuendelea na usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa Jamhuri Alhamisi.

Kabla ya kuendelea na usikilizwaji, mahakama hiyo ilikubali kupokea ripoti ya mkemia mkuu wa Serikali baada ya kufanyiwa uchunguzi sampuli ya mkojo wa Agnes.

Uamuzi huo ulitolewa kutokana na mawakili wa mshtakiwa huyo, Nehemia Nkoko na Simwanza, kupinga mahakama kupokea ripoti hiyo iliyokuwa inataka kutolewa na mkemia Elias Mulima ambaye alipima sampuli ya mkojo huo.

Baada ya kupokelewa kwa ripoti hiyo, shahidi huyo alihojiwa na wakili Simwanza, ambapo katika ushahidi wake aliieleza mahakama kuwa ana uhakika sampuli ya mkojo aliyoifanyia uchunguzi ilikuwa na Agnes.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles