26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 3, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Ndumbaro: Afrika inahitaji kauli moja uwindaji wanyamapori

Na Mwandishi Wetu, Cape Verde

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk.Damas Ndumbaro, amesema nchi za Afrika zinahitaji kuwa na kauli moja kuhusu taratibu  na bei  za wanyamapori  katika biashara ya uwindaji wa kitalii

Dk. Ndumbaro ametoa kauli hiyo a alipozungumza  kwa nyakati tofauti katika vikao na baadhi ya  mawaziri wa utalii wa nchi za Afrika  kwenye mkutano wa 64 wa  Kimataifa wa Utalii uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani  (INWTO) unaofanyika  uanoendelea nchini Cape Verde.

Amesema bei za wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa pamoja na vitalu vya uwindaji wa zimekuwa zikitofautiana kati ya nchi, hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli  za uhifadhi barani Afrika.

Akizungumza katika vikao hivyo na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe, Ngobhithize Ndlovu , amezitaka nchi hizo kuwa kitu kimoja katika kuamua na kupanga bei za uwindaji wa kitalii.

Amesema kutokana na kutofautiana kwa bei na baadhi  ya kanuni na taratibu hizo  wawindaji wa kitalii wamekuwa wakitumia mwanya huo  kuzikandamiza nchi za Kiafrika kwa kupanga bei wanazotaka wao, huku wakidai kuwa bei hizo za chini zimekuwa katika nchi nyingine pia.

” Utofauti wetu huu umekuwa ukitukandamiza kama nchi kwani tulitakiwa sisi tupange bei lakini kutokana na kutokuwa na umoja bei za wanyama  zimekuwa zikiamuliwa na wao  hili lazima tulikatae kwa kuungana kwa pamoja ” amesisitiza Dk.Ndumbaro.

Kufuatia hali hiyo, Dk.Ndumbaro amezitaka nchi zote zinazoendesha utalii wa uwindaji zifanye mkutano kwa njia ya mtandao ili kujadili mustakabali wa biashara hiyo na kisha  zitoke na kauli moja ili

kuwathibiti wawindaji wa kitalii kwa ajili ya maslahi mapana ya uhifadhi barani Afrika.

Amezitaja baadhi ya nchi wanachama wa SADC zinazofanya vizuri katika uwindaji wa kitalii kuwa ni Botswana, Zimbabwe pamoja, Zambia na Afrika ya Kusini.

Katika hatua nyingine , Dk.Ndumbaro ametoa ahadi kwa  nchi ya Zimbabwe  kama itakuwa  tayari ipewe mafunzo ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kiutalii kwa mfumo wa kidigitali ambao utasaidia kuongeza mapato maradufu

Amesema tangu kuanzishwa kwa mfumo huo nchini Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa nchi  ambapo wawindaji wa kitalii ili kuweza kupata vitalu vya uwindaji wamekuwa wakilazika kushiriki katika mnada wa kimtandao.

Naye, Ndlovu amesema nchi za kiafrika lazima ziungane katika suala hilo kwani katika nchi ya Zimbabwe wawindaji hao pia wamekuwa wakipanga bei huku wakidai kama hiyo bei haitawezekana watakwenda Tanzania ambako bei vitalu vya uwindaji ipo chini zaidi

Amesisitiza kuwa shughuli za uhifadhi zimekuwa ghali huku biashara hiyo ya uwindaji wa kiutalii ukibaki pale pale kutokana na kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine

Naye, Kamishna Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi amesema umoja huo wa nchi za Kiafrika katika biashara ya vitalu vya uwindaji italiingizia taifa fedha nyingi za kigeni sio kwa Tanzania pekee bali kwa Afrika nzima

” Biashara hiyo imekuwa na ushindani baina yetu bila kujuana kufuatia kila nchi kupanga bei zake kulingana na matakwa ya wadau hao huku shughuli za uhifadhi zikiwa juu zaidi” amesisitiza Kamishna Mabula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles