25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Dk. Ndugulile: Chloroquine inapunguza makali ya corona, haitibu

Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM 

NAIBU Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amesema dawa ya Chloroquine haitibu ugonjwa wa unaosababishwa na virusi vya corona  bali husaidia kupunguza ukali wa homa ya mapafu (pneumonia) hivyo kufupisha muda wa kuugua homa hiyo.

Amesisitiza kuwa hadi sasa hakuna dawa inayotibu ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo vya corona.

“Dawa hii tulitumia kutibu malaria na mwaka 2001 tulisimamisha matumizi yake baada ya kusababisha usugu wa malaria na sasa hazipo nchini kwetu.

“Utafiti uliofanyika nchini China unaonesha kuwa dawa hiyo haitibu Corona bali inapunguza makali ya homa ya mapafu tu na wagonjwa wanaotumia  ni wale ambao wana homa kali ya mapafu.

“Hivyo basi hawezi kupewa kila mtu wanapewa hao wenye homa ya mapafu kwa ajili ya kupunguza makali na nikiangalia kwa virusi vya corona kuna dalili zingine kama kukohoa, mafua, nimonia na zingine,”alifafanua Dk. Ndugulile.

Amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi hivyo na kuepukana habari za upotoshaji.

“Tunachosisitiza Wizara ya afya ni kila mmoja achukue tahadhari watu wanawe mikono kwa kutumia maji safi titirika na sabuni au vitakasa mikono,funika mdomo na pua  kwa kitambaa au mask kama unakohoa au kupiga chafya.

“Hakikisha haugusi  macho, pua, mdomo kwa mikono ambayo hujanawa, safisha sehemu inayoshikwa mara kwa mara na watu kwahiyo kila mtu azingatie tahadhari zinazotolewa na wahudumu wa afya,” alibainisha.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles