25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

DC Serengeti apiga marufuku minada, masomo ya ziada

Na MALIMA LUBASHA-SERENGETI

MKUU wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Nurdin Babu, amepiga marufuku ya mikusanyiko sehemu za minada, starehe za pombe na wanafunzi kwa ajili ya masomo ya ziada  ili kupunguza uwezekano wa maambukizi ya virusi vya corona hadi hapo Serikali itakapotoa tangazo lingine.

Hatua hiyo imetokana na kupatikana kwa wagonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya corona hapa nchini.

Akizungumza na gazeti hili Ofisini kwake, alisema Serikali tayari imekwishatoa maelekezo ya kufunga shule zote nchini, hivyo kuanzisha masomo ya ziada kipindi hiki cha mapumziko ni sawa na kuanzisha shule nyingine jambo alilosema ni kinyume na maelekezo yaliyotolewa.

“Serikali imeamua kufunga shule ili kuwaepusha wanafunzi na janga la corona wa madarasa ya awali, msingi ,sekondari hadi vyuo vikuu halafu watu waanzishe madarasa ya mtaani ambako tumezuia mikusanyiko ni hatari zaidi na ninawataka wazazi wachukue tahadhari,” alisema.

Pia amepiga marufuku minada kufanyika wilayani huo ikiwa ni pamoja na  mikusanyiko.

Pia amesisitiza kuzingatia kunawa mikono hasa katika sehemu za misikitini, makanisani, sokoni, baa, mikutano, semina na makongamano.

Babu amewaonya wananchi kuacha kutoa taarifa zisizo za kweli kwani hadi sasa wilaya haina mgonjwa mwenye maambukizi ya corona.

“ Kwa wale watakaokuwa na ulazima wa kusafiri nje ya wilaya wanapaswa kuchukua hatua za kujilinda na maradhi hayo…niwaombe wananchi kuepuka safari zisizo za lazima,” alisema Babu.

Aliwataka wananchi wanaokwenda sokoni ,hospitali kuona wagonjwa au magereza kusalimia jamaa na maeneo mengine ya kutafuta huduma kuepuka mikusnyiko na baada ya kupata huduma warudi nyumbani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,875FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles