27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mashinji aishukuru TAWA

Na Mwandishi wetu, Mtanzania Digital

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dk. Vincent Mashinji amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeendelea kuunga mkono jitihada za Baba wa Taifa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha elimu inakuwa kipaumbele wilayani Serengeti.

Hayo ameyasema Februari 1, 2024 wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na TAWA kwa kushirikiana na nguvu za wananchi kwa fedha zinazotokana na shughuli za uwindaji wa kitalii.

“TAWA moja kwa moja wameweza kugusa maisha ya wananchi katika jamii hasa katika masuala muhimu ambayo hata Baba wa Taifa aliyeanzisha haya mapori aliyasisitiza, suala la elimu.

” Kwa kumuunga mkono Rais TAWA wameweza kutujengea miradi 6 ambayo imejielekeza katika Sekta ya elimu,” amesema Dk. Mashinji

Ametaja miradi hiyo kuwa ipo katika Kata ya Sedeco, vijiji vya Bonchugu na Mbilikiri wamejenga chumba kimoja cha darasa huku Kata ya Kyambahi Kijiji cha Bokore wamejenga vyumba viwili (vya madarasa.

Pia katika Kata ya Manchira Kijiji cha Kazi wamejenga nyumba moja ya mwalimu na matundu 10 ya vyoo katika shule ya msingi Rwamchanga kikiwemo choo kwa ajili ya watu wenye ulemavu pamoja na chumba maalumu cha wanafunzi wakike kwa ajili ya kubadilishia taulo.

Aidha ameshukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Menejimenti ya TAWA kwa kurejesha rasilimali ambayo ni endelevu na kuhakikisha kile kidogo kinachopatikana katika uhifadhi kinarudi mikononi mwa wananchi.

Kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Kyambahi, Herman Kinyalire amemshukuru Rais Dk. Samia kupitia TAWA kwa kuwezesha ukamilishwaji wa miradi mikubwa minne katika Kata yake ambayo ni madarasa manne vyumba viwili vya madarasa pamoja na thamani za shule.

Aidha amesema utekelezaji wa miradi hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ujangili katika Kata yake na kuwafanya wananchi waongeze ushirikiano katika uhifadhi wa wanyamapori kwa kuwa wanaziona faida za moja kwa moja zinazotokana na shughuli za uhifadhi.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja amesema TAWA haiwezi kuongelea mafanikio wanayoyapata ikiwa ni pamoja utekelezaji wa miradi hiyo bila kuhusisha jitahada za dhati zilizofanywa na Dk. Samia alipocheza filamu maarufu ya Tanzania The Royal Tour ambayo imekuwa chachu ya ongezeko la watalii wa uwindaji katika hifadhi mbalimbali zinazosimamiwa na taasisi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles