24.8 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania, Chelsea zaanza mazungumzo ushirikiano wa kukuza vipaji

Na Brown Jonas

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Mratibu wa Klabu ya Chelsea ya England, Tajinder Sumal kuhusu uwezekano wa Tanzania kushirikiana na klabu hiyo katika kuibua na kukuza vipaji vya mchezo wa soka.

Mazungumzo hayo yamefanyika Februari 2, 2024 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Ndumbaro amemueleza Mratibu huyo kuwa Tanzania inaendelea kupiga hatua katika michezo kwani timu za soka za wanawake na wanaume ngazi ya klabu pamoja na Taifa zinafanya vizuri ikiwemo kuonesha ushindani katika Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) pamoja na Kombe la Mataifa Afrika kwa Wanawake (WAFCON) ambayo Tanzania imefuzu ikiwakilisha ukanda wa CECAFA.

“Tanzania ina vipaji vingi, tunatamani vipaji hivi viendelezwe, na tukipata wawekezaji kama hawa tunaonesha nia ya ushirikiano, kwa hiyo kupitia klabu hii, tumeanza mazungumzo na wataalamu wetu watakaa pamoja na kujadilliana na wakifikia makubaliano basi tutasaini mkataba wa ushirikiano” amesisitiza Ndumbaro.

Kwa upande wake Mratibu huyo Tajinder amesema amefurahishwa na vipaji vilivyopo nchini, pamoja uzuri wa nchi ambayo imejaa amani upendo na watu wakarimu. Huku akiahidi endapo watafikia makubaliano ya ushirikiano klabu hiyo itakua tayari kukuza na kuibua vipaji vya michezo pamoja na kufanya biashara kupitia michezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles