23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Dk. Mabula awatuliza wananchi

Na Munir Shemweta, WANMM HANDENI

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula amewatuliza wananchi wa Kijiji cha Sindeni wilayani Handeni mkoani Tanga kutokana na mgogoro kati yao na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuhusu mpaka baina ya kijiji cha Sindeni na Shamba la Miti la  Korogwe.

Dk. Mabula aliwatuliza wananchi hao, baada ya kufika katika shamba hilo kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi na nyumba za watumishi  wa  TFS zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga.

Aliitaka idara ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, ikisimamiwa na ofisi ya ardhi kanda ya kaskazini kuhakikisha inafanya uhakiki wa mpaka kati ya wakala huo na Kijiji cha Sindeni na kuweka alama ili kukomesha mgogoro huo unaozuka mara kwa mara.

‘Kitakachofanyika ni uhakiki wa mipaka ya kijiji chenu kinaishia wapi, TFS wanaishia wapi, NARCO wanaishia wapi, tutaheshimu mipaka na nyaraka zilizoanzisha vijiji vyenu,’’ alisema.

Uamuzi wa Dk. Mabula kutoa maagizo hayo, ulitokana na  wananchi kulalamika kuwa wakala huo, uliongeza eneo inalomiliki katika shamba hilo kwa kuingia ndani ya eneo la kijiji jambo linalochochea mgogoro.

Ally Mhina mkazi wa Kijiji cha Sindeni alisema  wakala huo iliacha eneo lake la asili na kuongeza eneo lingine.

Meneja wa Shamba la Miti la Korogwe, Pregreen Mushi alisema wenyeji wa Sindeni walivamia eneo la wakala, huku wale wa Kwamatuko na Kwaingoma wakiuza  maeneo ya hifadhi kwa jamii ya wafugaji na mkuu wa wilaya ya Handeni alishatoa agizo wote waliovamia kuondoka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alisema alishashughulikia mgogoro huo na kuwataka wasioridhika wasioridhika na utatuzi wake kwenda mahakamani na kufafanua kuwa katika jitihada zake za kutafuta suluhu ya mgogoro huo baadhi ya wananchi walikubali kuwepo msitu huo na sasa wananufaika kwa kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mustafa Beleko alisema pamoja maagizo ya naibu waziri  kuhusu uhakiki wa mpaka kati ya wao kama halmashauri watachukua ramani ya kijiji wakati wa uhakiki mipaka ili  kukomesha kuibuka kwa mgogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles