23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Jumbe aipa kongole STAMICO kuunga mkono uchumi wa buluu kupitia Rafiki Briquettes

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Wizara ya Uuvi na Uchumi wa Buluu, Dk. Aboud Jumbe ametembelea banda la STAMICO wakati wa ufungaji wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania (TGS) uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.

Wakati akiwa katika Banda la STAMICO leo Novemba 11, 2023 Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Zanzibar alipata maelezo ya shughuli mbalimbali za Shirika kutoka Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO CPA (T), Dk. Venance Mwasse.

Aidha, Dk. Mwasse alimwelezea Jinsi ya Shirika ilivyoingia Makubaliano (MoU) na Wizara ya Maji, Nishati na Madini kuifikisha nishati ya mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes kwa wananchi wa Zanzibar.

Amesema Novemba 13, 2023 kutakuwa na kikao kazi cha Mashirikiano kati ya STAMICO, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar na taasisi zingine za Serikali na wadau kwa ajili ya kujadili njia bora ya kuifikisha nishati hii kwa Wananchi.

Naye Katibu Mkuu Dk. Aboud Jumbe aliwashukuru STAMICO kwa ubunifu mkubwa wa uzalishaji wa nishati hiyo mbadala ya Rafiki briquettes inayozalishwa kutokana na mabaki ya makaa ya mawe.

Pia ameitaka STAMICO kushirikiana pia na Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu katika kuhakikisha nishati hiyo inawafikia wavuvi na wakaushaji dagaa ambao wanatumia gharama ni kubwa kutumia mkaa unaotokana na miti kwa ajili ya kukaushia dagaa.

Amesema wafanyabiashara hao hutumia mkaa wa miti kwa wingi na kuchochea uharibifu wa mazingira. Ameongeza kuwa kwenye kikao hicho cha Novemba 13, 2023 Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu inatakiwa kujumuika kwa dhati kama mmoja ya wadau wakubwa.

Awali, akitoa salamu kwa Washiriki wa Mkutano huo Dk. Mwasse aliwapongeza TGS kwa ubunifu wa kupeleka Mkutano mkuu Zanzibar. Amesema hatua hiyo imeifanya STAMICO kupata manufaa mbalimbali ikiwamo nafasi ya kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Zanzibar.

Aidha, amewapongeza TGS kwa mada nzuri zinazozungumzia madini ya kimkakati ambayo kwa sasa dunia inahamia huko katika utafiti wa madini hayo. Pamoja na mambo mengine, Dk. Mwasse alizungumzia ‘Dira 2030’ inayoenda sambamba na kauli mbiu kuwa Madini ni Maisha na Utajiri na kusisitiza kuwa dhana hiyo inajikita katika kutafuta taarifa za kijiolojia.

Amesema taarifa za sehemu yalipo maji, petrol, mafuta ya aina mbalimbali ikiwamo madini na gesi, zitafahamika na kusaidia nchi kwenye shughuli mbalimbali za uchimbaji.

Dk. Mwasse pia aliwaasa washiriki na viongozi wa TGS kuiishi dira hiyo ambayo awali ilipata baraka kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na sasa STAMICO vilevile inaendelea kuiishi dira hiyo na kuhakikisha inafanikiwa.

Mkutano huu wa jiolojia Tanzania ambao umeambatana na maonesho umefungwa rasmi leo Novemba 11, 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles