27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Djomaly ateuliwa kuwa bosi wa tuzo za Zikomo Awards nchini Zambia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Patrick Djomaly ambaye ni Meneja wa Kimataifa wa Mwanamuziki wa Muziki wa Dansi nchini, Christian Bella, amepata nafasi ya kuwa Mkurugenzi mpya wa tuzo kubwa nchini Zambia zinazofahamika kama Zikomo Awards.

Djomaly ambaye kwasasa anaishi nchini Marekani, ameiambia Mtanzania Digital leo Agosti 19, 2022 kuwa miongoni mwa vitu ambavyo vitaboreshwa kwenye tuzo hizo zitakazotolewa Oktoba 15, mwaka huu jijini Lusaka, Zambia ni vipengele vya Sayansi na Teknolojia.

Akizungumzia tuzo hizo, Djomaly amesema: “Mpango wa tuzo za Zikomo Awards ni kuwajengea uwezo wasanii waliosahaulika, wajasiriamali, wapenda ubinadamu na kimsingi kila mtu katika tasnia ya burudani, nikiwa Mkurugenzi wa Zikomo Awards tuligundua kuwa kuna watu wengi wanaostahili kutambuliwa lakini hawapati hiyo nafasi kutokana na jinsi tasnia ilivyo na upendeleo.

“Kila mtu kwenye tasnia anastahili kuthaminiwa kwa juhudi pamoja na kupewa heshima, matarajio yangu ni kwamba Zikomo African Awards inakwenda kuwa chapa ya Kimataifa, hadi sasa tumeweza kujumuisha nchi nyingi za Afrika na kwa sababu huu ni msimu wa pili na kutakuwa na mengi kwa ajili ya Afrika,” amesema Djomaly.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles