27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

Asasi za Kiraia ni nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo- Nsekela

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Imeelezwa kuwa jitihada za makusudi zinazofanywa na Asasi za Kiraia katika kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali wa sekta hiyo zinatambuliwa na sekta binafsi kama sehemu muhimu ya kuharakisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) 2022, Agosti 18, jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 18, 2022 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela katika uzinduzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) 2022 ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Nsekela amesema kuwa ushirikiano baina ya Asasi za kiraia na Sekta Binafsi unaweza kutoa suluhisho la changamoto za maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ufanisi zaidi kuliko kila Taasisi kufanyakazi kivyake.

“Kwa bahati mbaya kumekuwepo na ushirikiano usioridhisha kati ya Asasi za Kiraia na Sekta Binafsi katika kutatua changamoto za kimaendeleo nje ya ushirikiano wa kiufadhili. Hata hivyo, sisi ni wamoja. Ushirikiano kati ya sekta mbalimbali miongoni mwa mashirika, taasisi na wananchi ni miongoni mwa hatua zinazohitajika kuchukuliwa. Tunajenga Taifa moja na jamii moja ya kimataifa. Tunajenga simulizi zetu kwa ajili ya maendeleo yetu.

“Katika Sekta Binafsi tunaongelea uwekezaji unaoleta matokeo chanya. Huu ni uwekezaji unaofanywa kwa lengo la kuleta matokeo ya kijamii au kimazingira yanayopimika mbali na faida za kifedha. Lengo ni kuleta maendeleo ya kijamii na uthabiti wa kiuchumi. Msisitizo wa uwekezaji wenye kuleta matokeo chanya kijamii ni msingi muhimu wa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya sekta binafsi na asasi za kiraia. Hii pia inaakisi Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Malengo Endelevu ya Maendeleo,” amesema Nsekela.

Mratibu wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI), Justice Rutenge, akizungumza katika hafla hiyo kuelezea matukio mbalimbali yatakayofanyika katika Wiki AZAKI ya 2022 yatakayofanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 24, 2022 mpaka Oktoba 28, 2022.

Wiki ya Asasi za Kiraia ya 2022 inawaleta pamoja washirika muhimu wa maendeleo na ina lengo la kuimarisha ushirikiano wenye lengo la kukuza ushiriki wa Asasi za kiraia katika maendeleo ya Tanzania, kuimarisha hatua za pamoja zenye lengo la kufanyia kazi changamoto za kimaendeleo na kubadilishana mawazo kuhusu changamoto hizo.

Kuhusu Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI), Nsekela amesema, “Tunaisubiri kwa hamu Wiki ya Asasi za kiraia ya mwaka huu. Tujikite zaidi katika kuoanisha uwekezaji wa Sekta Binafsi na maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi. Uwekezaji wenye kuleta matokeo chanya ya kijamii ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha uwekezaji huo unaleta maendeleo endelevu.

“Tusherehekee maendeleo ya watu kupitia simulizi za mabadiliko yaliyofanikishwa kwa kiasi kikubwa na Asasi za kiraia, lakini pia tuje na njia mpya za kuwekeza katika mipango ya kijamii kupitia ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali,” amesema Nsekela.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Anna Henga, amezungumzia kwa ufupi historia ya Wiki ya Asasi za Kiraia.

“Ujumbe wa mwaka 2018 ulikuwa ni ‘Ukuzaji wa Viwanda Tanzania: Watu, Sera na Utekelezaji’. Mwaka 2019 ujumbe ulikuwa ni ‘Maendeleo Kupitia Ushirikiano: Ushirika Kama Chachu ya Maendeleo Tanzania’, na mwaka 2021 ulikuwa ni ‘Mchango wa Asasi za Kiraia kwa Maendeleo ya Taifa’. Tangu kuanzishwa kwake, kumekuwa na utambuzi unaoongezeka miongoni mwa wadau wa umuhimu wiki hii kama jukwaa muhimu linalowakutanisha wadau mbalimbali.

“Sisi sote ni mashahidi wa umuhimu na matokeo chanya ya Wiki ya Asasi za Kiraia tangu ilipoanzishwa, ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa umoja na mshikamano miongoni mwa wadau wa maendeleo nchini. Wiki ya Asasi za Kiraia pia imeleta mwamko mkubwa miongoni mwa washirika wa maendeleo wa umuhimu wa kuionyesha jamii mchango wao katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Wiki hii huweka msisitizo katika umuhimu wa ufanyaji kazi wa pamoja na ushirikiano katika kuwafikia wananchi,” amesema Henga.

Naye Mratibu wa Wiki ya Asasi za Kiraia, Justice Rutenge, amesema ajenda ya wiki ya mwaka huu itajikita katika kuhakikisha washirika katika sekta mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles