DIVA: NAJUTIA KUWA VIDEO QUEEN

0
1053

NA JESSCA NANGAWE


STAA wa Bongo Fleva, Lulu Abass maarufu kama Lulu Diva, amesema moja ya mambo anayojutia maishani mwake ni kupitia kwenye kazi ya video queen.

Lulu Diva ambaye kwa sasa anafanya vyema na kibao cha ‘Amezoea’, amesema kupitia kwenye kazi hiyo hakuweza kufanikiwa lolote zaidi ya kufahamika na kuchukuliwa kwa mtazamo hasi na jamii.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Lulu Diva, alisema kazi hiyo ni moja ya mambo anayojutia na endapo angefahamu tangu awali asingeweza kufanya.

“Unajua video queen wengi wanatutafakari kama ni kazi ya kujiuza, nilipitia na ukweli kwa sasa najuta, ingawa ilinifanya kujulikana lakini haikuweza kunilipa kwa lolote zaidi ya kujijengea picha mbaya kwa jamii, nashukuru Mungu kwa sasa muziki wangu unafanya vyema nimeendelea kukubalika,” alisema Lulu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here