23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

HALMASHAURI ZA LINDI, KILWA ZATAKIWA KULIPA MADENI YA WAKANDARASI

Hadija Omary, Lindi

Bodi ya Barabara Mkoa wa Lindi, imeziagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na Kilwa kulipa malimbikizo ya madeni ya Sh milioni 15.3 ambazo zilikuwa ni fedha za matazamio za wakandarasi.

Hayo yameibuka katika taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Lindi kubaini kuwa miongoni mwa changamoto zinazokwamisha utekelezwaji wa majukumu ni malimbikizo mengi ya madeni ya wakandarasi ambao wamefanya kazi katika baadhi ya Halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2015/216 na 216/2017.

Mhandisi Msaidizi TARURA Mkoa wa Lindi, Aloyce Nombo amesema fedha hizo ni za matazamio ya wakandarasi ambazo zilitakiwa kuhamishwa kwenye akaunti ya amana za halmashauri na kuingizwa katika akaunti za TARURA  ambapo Halmashauri ya Kilwa inadaiwa kiasi cha sh.81,183,370 huku halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ikiwa na deni la sh.72,338,270.

“Ziko changamoto nyingi zinazoikabili ofisi TARURA ikiwamo ukosefu wa magari ya usimamizi hasa kwa Halmashauri ya Kilwa, Liwale, Nachingwea na Lindi pamoja na ukosefu wa vyumba vya kutosha kwa ajili ya ofisi,” amesema Nombo.

Hata hivyo, Nombo amesema kwa kushirikiana na Katibu Tawala Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Mratibu na Mameneja wameweza kuzikabili na kufanya kazi ziweze kufanyika kwa ufasaha.

Nombo pia amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 TARURA Mkoa wa Lindi umetengewa fedha Sh bilioni 7.4 ambapo Sh bilioni saba ni kwa ajili ya matengenezo na usimamizi wa miradi ya barabara na Sh milioni 4.2 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Zablon Bugingo amesema Halmashauri yake inalitambua deni hilo na mkakati walionao kwa sasa ni kulipa ambapo tayari wameshaingiza kwenye bajeti ya 2018/19.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles