26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Dili la Neymar kutua Barcelona lakwama

BARCELONA, HISPANIA

MIPANGO ya timu ya Barcelona kumrudisha mchezaji wao wa zamani Neymar inaweza kuwa migumu katika kipindi hiki cha kiangazi baada ya PSG kukataa ofa ya pauni milioni 74 pamoja na kiungo mshambuliaji Philippe Coutinho.

Uongozi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Hispania mapema wiki hii walifunga safari kwa ajili ya kwenda kumalizana na uongozi wa timu hiyo, lakini inasemekana kuwa PSG bado walikuwa wanahitaji kiasi cha fedha kiongezeke pamoja na wachezaji wawe wawili badala ya mmoja Countinho.

Rais wa timu ya Barcelona, Josep Bartomeu alikutaka na bosi wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi jijini Liverpool, kwenye mkutano wa viongozi wa timu za Ulaya.

Viongozi wa Barcelona wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanaipata saini ya mchezaji huyo katika kipindi hiki cha kiangazi kutokana na mchezaji huyo ambaye aliondoka Barcelona mwaka 2017, kwa sasa hana maelewano mazuri na uongozi wa mabingwa hao wa nchini Ufaransa.

Hata hivyo, wapinzani wa Barcelona nchini Hispania, Real Madrid, wapo katika vita hiyo ya kuwania saini ya mchezaji huyo raia wa nchini Brazil. Wakala wa mchezaji mapema wiki hii alionekana katika viwanja vya Santiago Bernabeu kwa ajili ya kutaka kufanya mazungumzo na uongozi wa Madrid juu ya uhamisho wa mchezaji huyo.

Inasemekana kuwa, Barcelona wanajipanga tena kutuma ofa ya mwisho ya kiasi hicho cha fedha pamoja na wachezaji wawili ikiwa Coutinho pamoja na kiungo mwingine Ivan Rakitic.

Hata hivyo kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya habari nchini Ufaransa, PSG wanawataka Barcelona kuhakikisha wanaweka mezani kiasi cha pauni milioni 206 ili kuweza kukamilisha dili hilo, alini wakishindwa kabisa kuweka kiasi hicho cha fedha basi waweke mezani pauni milioni 93 pamoja na Coutinho, Rakitic na Nelson Semedo, ila Barcelona hawataki kumjumlisha na Semedo.

Tangu Neymar ajiunge PSG, amecheza jumla ya michezo 58, akifunga jumla ya mabao 51, akitoa pasi za mwisho 29, akioneshwa kadi 14 za njano na moja nyekundu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles