Dida aweweseka matokeo Yanga

IMG_0762

Na THERESIA GASPER -DAR ES SALAAM

KIPA wa timu ya soka ya Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, amesema hawajafurahia matokeo ya sare ya bao 1-1 waliyopata juzi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana.

Mchezo huo wa tatu wa Kundi A kwa upande wa Yanga walioambulia pointi moja, ulichezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Dida alisema hawawezi kukata tamaa hadi hatua ya mwisho kwa kuwa wanaamini watafanya vizuri katika mechi zinazofuata.

“Ninawaomba mashabiki wa Yanga wasikate tamaa kutokana na matokeo yasiyoridhisha bali waendelee kutupa sapoti kwani kuna mechi tatu mbele zinaweza kuwarudishia furaha,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here