26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mahadhi amuibua Msuva Yanga

IMG_0676

Na ADAM MKWEPU -DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa timu ya Yanga, Juma Mahadhi, amesema ubora wake uwanjani umechangia kuongeza changamoto kwa kiungo, Simon Msuva na kufahamu majukumu yake ndani ya timu hiyo.

Mahadhi alijiunga na Yanga akitokea timu ya Coastal Union ya Tanga  ambayo ilishuka daraja  msimu uliopita licha ya kuisaidia ibaki katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa mara ya kwanza, Mahadhi aliichezea Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuonyesha uwezo mkubwa uliowavutia mashabiki wengi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mahadhi alisema juhudi alizoonyesha katika mchezo wake wa kwanza wa kimataifa ndio zimemfanya Msuva azinduke na kufanya mazoezi kwa bidii ili aweze kutetea namba yake uwanjani.

“Nilipata nafasi adimu nikaitendea haki na kuifanyia kazi kwa uhakika kwa sababu Msuva alikuwa anaumwa, lakini nina malengo ya kucheza soka barani Ulaya, hivyo nitajitahidi ili msimu ujao nifike mbali zaidi ya Yanga,” alisema.

Mahadhi alisema hawezi kutumia nguvu nyingi ili kupata namba kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwa anaamini kipaji chake kinampa nafasi ya kuendelea kuaminiwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi Hans van der Pluijm.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles