24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama za mwanzo sasa kuboreshwa

 Jaji Othman Chande
Jaji Othman Chande

NA JANETH MUSHI, ARUSHA

MAHAKAMA 18 za mwanzo katika mikoa ya Arusha na Manyara ambazo zimefungwa kutokana na miundombinu yake kuchakaa, zinatarajiwa kukarabatiwa kupitia mkakati wa kitaifa wa kuboresha majengo ya mahakama nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jijini hapa juzi na Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Othman Chande, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha.

Jaji Mkuu alifanya mkutano huo baada ya kumaliza kikao chake na majaji, mahakimu na watumishi wa mahakama za mikoa hiyo.

Kwa mujibu wa Jaji Chande, mkakati wa kufufua majengo ya mahakama ambayo hayatumiki kutokana na uchakavu, utatekelezwa kwa ushirikiano na halmashauri za wilaya husika.

“Zaidi ya asilimia 70 ya majengo ya mahakama hapa nchini, hayamilikiwi na mahakama kwani yamekodiwa. Kwa hiyo kupitia mkakati huo tutayalinda maeneo yote ya mahakama kwa kuyawekea uzio ili yasivamiwe na wananchi,” alisema Jaji Chande.

Jaji Chande alizitaja mahakama hizo zilizoko Wilaya ya Arumeru kuwa ni Ngarenanyuki, Nkoaranga, Oldonyosambu, West Meru na Usa  River. Nyingine ni Makuyuni na Engaruka zilizoko Wilaya ya Monduli na Nainokanoka na Enduleni zilizoko Wilaya ya Ngorongoro, Mkoa wa Arusha.

Kuhusu mahakama za Mkoa wa Manyara katika Wilaya ya Babati alizitaja kuwa ni Gidasi, Minjingu na Gendikuu na katika Wilaya ya Mbulu alisema ni Magandi, Kainamu, Tumati, Muralina na Tilawi. Katika Wilaya ya Simanjiro aliitaja Mahakama ya Terati kuwa ndiyo itakayokarabatiwa.

Akizungumzia suala la utendaji kazi, alisema mahakimu waliokaa kwenye vituo vya kazi kwa muda mrefu, watahamishwa katika vituo hivyo ili wakafanye kazi katika maeneo mengine.

“Tunatamani hakimu akae kituo kimoja labda kwa miaka minne ila kutokana na uwezo wa fedha, inabidi tuwahamishe kwa mpango ila tumesema hawa wa muda mrefu tutawahamisha kwenye mikoa mingine au ndani ya mkoa aliopo ili apate uzoefu mwingine,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles