23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Diamond, Kiba wapongezwa bungeni

Ramadhan Hassan -Dodoma

SERIKALI imewapongeza wasanii, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Salehe a.k.a Kiba kwa kuitangaza na kuipeperusha  vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi.

Hayo yalielezwa jana bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harisson Mwakyembe wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2020-2021.

Waziri Mwakyembe alisema  kwa kuzingatia ubunifu uliotukuka, wasanii wa Tanzania wameweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ikiwa ni pamoja na kuitangaza nchi.

Aliwataja wasanii wengine walioitangaza vyema nchi  kuwa   ni Rajabu Abdul Kahali ‘Harmonize’, Vanessa Mdee, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Sharif Thabeet  ‘Darassa’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na wengine wengi.

 “Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana wasanii hawa na kuwaasa  wengine kuongeza kasi na ubunifu katika kazi zao ili zivutie masoko ya ndani na nje ya nchi,” alisema Mwakyembe.

Aliongeza kuwa Baraza la  Sanaa ya Taifa (BASATA)  limetoa jumla ya vibali 1,620 kwa wasanii wa Tanzania kwenda nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa hadi Machi, 2020.

Pia katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 vibali vilivyotolewa na BASATA kwa muktadha huo ni 135.

Vilevile, Baraza limetoa jumla ya vibali 527 kwa wadau kuingiza wasanii wa nje ya nchi kufanya shughuli za sanaa nchini ili kujifunza sanaa ya Tanzania ambapo vibali 25 vimetolewa katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi, 2020.

Pia Baraza kwa kushirikiana na ubalozi wa India nchini, lilipeleka kikundi cha sanaa cha Lumumba Theatre Group kushiriki katika Tamasha la 34 la Kimataifa la kazi za Sanaa lililofanyika Surajkund nchini India.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles