Barnaba awakubali Makamua, Joslin

0
1161

GLORY MLAY

STAA wa Bongo Fleva, Elias Barnaba ‘Barnaba’, amesema mpaka sasa ndani ya muziki huo hawajatokea wasanii wenye uwezo mkubwa kama Makamua na Joslin.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Barnaba anayetamba na wimbo mpya, One In A Million alisema licha ya wasanii hao kuwa kimya kwa sasa lakini hakuna msanii aliyeweza kufikia viwango vyao.

 “Ni wasanii ambao walikuwa na sauti za kipekee, kila walichokuwa wanakiimba kinaeleweka na mpaka sasa nyimbo zao ukizisikiliza utadhani zimetungwa jana, ni tofauti na wasanii wengi ambao kazi zao hupotea muda mfupi baada ya kutoka,” alisema Barnaba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here