R.Kelly aomba tena kutolewa jela

0
837

Chicago, Marekani

MFALME wa RnB duniani, Robert Kelly ‘R.Kelly’, ameiomba tena Mahakama mjini Chicago imruhusu kutoka jela baada ya mmoja ya wafungwa kwenye gereza alilofungwa kukutwa na maambukizi ya corona.

Kelly ambaye yupo kwenye jela ya Chicago Metropolitan Correctional Center, ameshikiliwa kwenye gereza hilo kwa makosa mbalimbali ya kudhalilisha wasichana kingono.

Aidha mkali huyo alishatuma ombi hilo kwa Jaji Ann Donnelly ambaye  alilikataa kwa madai kuwa Kelly hayupo kwenye kundi la hatari ya kupata corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here