27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

DC Jokate kusimamia ujenzi msikiti Kisarawe

Na MWANDISHI WETU-PWANI

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jakate Mwegelo, ameahidi kusimamia ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa wilaya hapa ambao ujenzi wake utakamilika katika kipindi cha mwaka mmoja.

Msikiti huo wa kisasa wa ghorofa mbili unajengwa wilayani hapa kwa gharama ya Sh milioni 500, ambapo DC Jokate aliombwa kuwa mlezi katika ujenzi huo kutokana na nafasi yake.

Akizungumza na waumini wa dini hiyo wilayani hapa, Jokate Mwegelo amesema katika maisha yake hakuwa akifikiria kuna siku moja atapata heshima ya kuwa mlezi wa msikiti na kuombwa kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa msikiti lakini wananchi wa Kisarawe wamempa heshima hiyo ambapo amesisitiza hatawaangusha na atashirikiana nao bega kwa bega hadi msikiti ukamilike.

“Nimefurahi sana kwa heshima kubwa mliyonipa ya kuwa mlezi wa kamati yenu ya ujenzi yenye kuratibu shughuli za ujenzi wa Msikiti wa Islamiya Kisarawe na niseme kwa dhati ya moyo wangu ahsante sana, nimeridhia kuwa mlezi na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu jinsi atakavyotuongoza naaamini sitowaangusha. Tutafanikisha ujenzi wa msikiti wetu huu wa Wilaya ya Kisarawe ambao utakuwa taaswira ya misikiti mingine ndani ya Wilaya yetu.

“Sisi sote tunafahamu msikiti ni taasisi inayojishughulisha na mambo mbalimbali ya kimaisha katika jamii ni pamoja na shughuli za maendeleo,kiuchumi na kiutamaduni na kwa mantiki hiyo kuwa na jengo la msikiti ni jambo muhimu katika kuratibu utekelezaji wa shughuli hizo,” amesema Jokate 

Amesema hata katika maandiko ya vitabu vitakatifu kama Korani inaeleza kwamba Mwenyezi Mungu humpenda mja wake anayejituma katika kufanya kazi, hivyo akiwa mlezi wa kamati iliyoundwa kushughulikia ujenzi atajitajidi kadri Mungu atakavyomuwezesha kutoa mchango wake wa hali na mali kufanikisha ujenzi huo kwa wakati.

“Pamoja na kuzungumzia ujenzi wa msikiti huu, sote tunafahamu kwamba tuko kwenye kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28, 2020, hivyo nitoe rai kwenu Kisarawe, dini zote na wananchi wote kuzingatia amani na utulivu. Sitarajii uvunjifu wa amani ndani ya Wilaya ya Kisarawe,” amesema 

Awali  akisoma risala kuhusu ujenzi wa msikiti huo, Katibu wa Msikiti wa Wilaya ya Kisarawe, Mohamed Bakari amesema kwamba wazo la kuujenga msikiti huo ili uwe mkubwa wa kisasa lilianza mwaka 2000, na eneo lilipatikana mwaka 2006 na ilipofika mwaka 2007 wakapata ramani na ujenzi ukaanza mwaka 2018.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles