27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Sh milioni 335 kuboresha huduma Mloganzila

Na AVELINE KITOMARY  -DAR ES SALAAM 

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili – Mloganzila imepokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Sh milioni 335 kutoka kwa Taasisi inayojihusisha na masuala ya afya ya Korea Kusini (KOFIH) kusaidia kuboresha huduma.

Akipokea msaada huo jana Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Profesa Lawrence Museru, alisema hospitali hiyo imekuwa na ushirikiano na taasisi hiyo tangu mwaka 2017 hivyo msaada huo ni matunda ya ushirikiano wao.

“Ushirikiano uliopo kwa sasa kati ya taasisi hizi mbili ni kujenga uwezo kwa Hospitali ya Mloganzila katika maeneo makuu mawili ambayo ni mafunzo na vifaa tiba. 

“Tumekabidhiwa vifaa vikijumusha vya kufanyia upasuaji vilivyogharimu Sh milioni 96 na vya ufundi kwa ajili ya matengenezo ya vifaa tiba vyenye gharama ya Sh milioni 235,”alisema Profesa Museru.

Alisema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza nguvu katika upasuaji wa masikio, pua na koo katika hospitali hiyo.

“Kuna vifaa vya kufanya upasuaji wa mafindofindo na nyama za pua seti sita, vifaa vya uchunguzi wa masikio na koo seti mbili, vifaa vya kufanyia upasuaji wa masikio na upandikizaji wa vifaa vya usikivu masikio seti nne.

“Vifaa vya upasuaji wa koo kwenye njia ya hewa seti tatu na vingine vingi tu,”alisema. 

Profesa Museru alisema pia wamekuwa wakishirikiana katika kuwapatia mafunzo wataalamu wa afya katika idara mbalimbali. 

“Taasisi hii imetusaidia kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya, tumepata madaktari bingwa kutoka katika vyuo mbalimbali vya Korea Kusini na hata sasa tunao madaktari wao wanaowajengea uwezo madaktari wetu,”alisema.

Kwa upande wake Naibu Mwakilishi Mkazi wa KOFIH, Kim Jungyoon, alisema taasisi hivyo itaendelea kushirikiana na hospitali hiyo ili kuboresha huduma za afya nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles