23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

DC ataka walimu, dobadoba wabanwe kukomesha mimba za utotoni

Gurian Adolf, Sumbawanga

MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Said Mtanda, ameshauri miongoni mwa wanaume ambao ni muhimu kuwabana ili kukomesha mimba za utotoni ni walimu na waendesha bodaboda kwani wamekuwa wakihusika kwa kiwango kikubwa kuwapa mimba wanafunzi.

Ushauri huo aliutoa jana wakati akichangia rasimu ya mkakati wa kukabiliana na mimba za utotoni katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) iliyowasilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,  Bonifas Kasululu.

Alisema hivi karibuni kumekuwa na kesi nyingi za walimu wakikuhusika kuwapa mimba wanafunzi kitendo ambacho kinahitaji jitihada ya kukabiliana nacho.

Alisema pia wanao endesha boda boda ni kundi jingine ambalo linahusika kutokana na vitendo vya kuwapa lifti wanafunzi wanapo kwenda na kutoka shule, na kuwanunulia zawadi ikiwemo chipsi kutokokana na njaa wanazokuwa nazo wanafunzi pindi wanapotoka shule.

Miingoni mwa mikati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, kumaliza tatizo hilo ni kila kijiji kwa na shule ya msingi na kila kata iwe na shule ya sekondari.

Alisema mkoa mzima una vijiji 59 ambavyo havina shule za msingi ambapo katika Wilaya ya Kalambo kuna vijiji 14, Nkasi vijiji 17 halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga vijiji 28 na halmashauri ya Manispaa hakuna kijiji kisichokuwa na shule.

Alisema katika mkoa mzima kata 25 hazina shule za sekondari ambapo alisema katika wilaya ya Kalambo zipo kata nane, wilaya ya Sumbawanga vijijini kata 10 Nkasi kata sita na Sumbawanga Manispaa kata moja.

Alisema kutokana na rasimu hiyo ambayo imepitishwa na kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa, anamatumaini kuwa katika kipindi cha miaka 10 suala la mimba za utotoni na kwa wanafunzi litabaki historia katika mkoa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles