20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

DC AAGIZA VICHANGA KUCHUNGUZWA UKEKETAJI

NA RAPHAEL OKELLO-BUNDA


MKUU wa Wilaya (DC) ya Bunda, Lydia Bupilipili, ameagiza wahudumu wa afya na madaktari wilayani hapa kuhakikisha  wanawafanyia uchunguzi watoto wote wachanga wanaofika kwenye kliniki, vituo vya afya na zahanati kama wamefanyiwa ukeketaji.

Hatua hiyo inatokana na madai ya kuwapo kwa vitendo vya ukeketaji wilayani hapa, ambavyo hufanyika kwa siri hasa kwa watoto wachanga mara tu wanapozaliwa.

“Ukeketaji ni ukatili, ni jambo lisiloweza kuvumilika, kwahiyo natoa agizo kwa madaktari na wauguzi fanyeni uchunguzi na kwa wale wote watakaobainika kuwafanyia ukeketaji watoto wachanga sheria

ichukue mkondo wake,” alisema Bupilipili.

Awali akiwasilisha taarifa ya hali ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wilayani Bunda, Mkurugenzi wa Shirika la Zinduka, Maximilian Madoro, alisema ukeketaji unafanyika kwa usiri mkubwa tofauti ilivyo katika wilaya za Tarime na Serengeti.

“Ukeketaji katika Wilaya ya Bunda hauambatani na sheria na matangazo kama ilivyo katika wilaya nyingine na ili kubaini

hali hiyo uchunguzi wa kina unatakiwa kufanyika kuhusu hali ya ukeketaji wa watoto wa kike,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Kuwakagua vichanga Ukeketaji sawa lakini bado kuna wanafunzi wanaofanyiwa ktk umri mbali mbali; akina mama wajawazito kufanyiwa na TBA au nurse aliyepewa hela anamfanyia wakati anapojifungua. Anadhania ni uchungu wa kuzaa lakini kumbe anakeketwa pia kwa vile alikwepa. Ndoa za muingiliano zinafanikisha FGM ktk umri mkubwa kwa makabila yasiyokeketa. Kukagua vichanga kutafanya akina mama wengine waliowakeketa wasiende kliniki. Elimu itolewe na kutumiwe picha na video ktk kuelimisha watu waone madhara ya FGM waache kufundisha Imani potofu. Wengine wanakeketa maiti ili akapokelewe huko kwani alikuwa hajaingia mila kukidhi matakwa ya wahenga. Ngariba wanaletwa mijini kama DSM wanakeketa kwa siri wasichana wa makabila yao kwa makundi. Research zimeonyesha hata Ulaya kama UK ngariba toka Nigeria wanapelekwa. Akina bibi wazee ndani ya familia ndio kazi yao wengine wanakata hovyo macho hayaoni wanaondoa hata vile mila haviondoni. Takwimu za ukeketaji TZ sio za kweli kwa sababu hatufanyi patient blinded medical research kuchukuza ukeketaji across the nation. Tunahoji sample au kuchunguza watoto. Serikali ihakikishe inaweka dawa za kutosha zahanati, vituo vya afya na hospitali zinazotibu maradhi ambayo husababisha watu wakekete as a preventive and curative measure kuifanya FGM ikomae na kukua. Uchafu wa nguo, mazingira, maji na mitandao ktk ngono ni matatizo yanayofanya ukeketaji usiishe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles