25.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 31, 2023

Contact us: [email protected]

Dawa nguvu za kike sokoni Septemba, madaktari wazungumzia ukubwa wa tatizo nchini

MWANDISHI WETU –Dar es Salaam

SHIRIKA linalohusika na udhibiti wa chakula na dawa nchini Marekani (FDA), limetoa dawa ya kutibu tatizo la ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), dawa hiyo itaanza kupatikana katika baadhi ya maduka ya dawa Septemba.

Taarifa hiyo ilisema dawa hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Palatin Technologies na kuruhusiwa kuuzwa na Amag Pharmaceuticals.

HALI ILIVYO NCHINI

Akizungumzia sababu zinazosababisha wanawake wakose hisia na tendo la ndoa, daktari wa wanawake kutoka Hospitali ya Palestina – Sinza, Dar es Salaam, Dk. Ali Njama, alisema tatizo kubwa linasababishwa na msongo wa mawazo.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni maradhi. Kwamba asilimia kubwa ya wanawake wakiwa wanaumwa hawana hisia za kufanya tendo la ndoa.

“Sababu kubwa ni msongo wa mawazo, kuna vitu anakuwa amevishikilia moyoni ambavyo labda alikwazwa na mpenzi wake, anakuwa hana furaha, labda kwa ugumu wa maisha.

“Nyingine ni maradhi, ugomvi wa mara kwa mara na mpenzi wake, hivyo zote hizo na nyingine zinamfanya akose hamu ya kufanya tendo la ndoa,” alisema Dk. Njama.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk. Muzdalfat Abeid, alisema hakuna tafiti zozote zilizofanyika kuthibitisha tatizo hilo.

“Hizi kesi sisi hatuna na hakuna tafiti zozote zilizofanyika, yaani kama wapo wanaokuja kusema hayo ni wachache sana, kwa ujumla hili si ‘common’,” alisema.

INAVYOTUMIKA

Taarifa hiyo ilisema dawa hiyo hutumika kupitia sindano ambayo husisimua njia ya akili inayotumika katika hisia za kushiriki tendo la ndoa.

Vilevile ilisema ukosefu wa hisia husababishwa na mwanamke kutoshiriki katika vitendo vinavyoweza kuvutia hisia za kushiriki tendo hilo.

“Kemikali kwa jina la Vyleese imejaribiwa kutengeneza kile ambacho kinaweza kuitwa viagra ya kike.

“Hili ni suala tata kwa baadhi ya wataalamu wanahoji asili ya tatizo la hisia za kingono na kukosa ukosefu wa msisimko wa mapema wakati mwathiriwa anapotumia.

“Ikilinganishwa na dawa nyingine, dawa hiyo haifanyi kazi katika mfumo wa mishipa, huongeza hamu ya tendo la ndoa katika mfumo wa neva,” ilieleza taarifa hiyo.

Vyleesi itashindana na Addyi ya watengenezaji dawa wa Sprout, dawa ya kila siku ambayo iliidhinishwa mwaka 2015 na watumiaji hawaruhusiwi kutumia pombe wakati wanapoitumia.

Addyi iliidhinishwa baada ya kufanyika kampeni ya pamoja na kukosolewa na wanasayansi wa FDA ambao wanaitambua kuwa na utendaji kazi wa kadiri na isiyo salama.

Tofauti na Addyi,Vyleesi haizuii matumizi ya pombe na inadaiwa kutoa fursa kubwa ikilinganishwa na mshindani wake, ikiwa na athari za chini na kwamba si lazima kutumia kila siku.

Athari zilizoonekana wakati wa majaribio yake ni pamoja na kichefuchefu ambacho hakikuchukua zaidi ya saa mbili na kilitokea baada ya matumizi ya dawa hizo,

Taarifa hiyo ilisema dawa hiyo hutumika kupitia sindano tumboni dakika 45 kabla ya tendo la ndoa.

FDA inapendekeza kwamba wagonjwa hawawezi kudungwa zaidi ya dozi moja katika saa 24 na si zaidi ya dozi nane kwa mwezi.

Nchini Marekani, tatizo hilo linawaathiri wanawake milioni sita, lakini ni wachache wanaotafuta tiba.

UTATA

Hata hivyo shirika hilo linatambua kwamba halijui jinsi Vyleesi inavyofanya kazi akilini ili kusisimua hisia za tendo la ndoa.

Upungufu wa hisia za tendo la ndoa unaweza kusababishwa na matatizo ya nje, kimaungo na kiakili, kulingana na wataalamu tofauti.

Dawa hiyo ya Vyleesi pamoja na usalama wake, ilijaribiwa katika wiki 24 ikishirikisha zaidi na wanawake 1,200 ambao hawajafikia ukomo wa hedhi.

Wagonjwa wengi walitumia dawa hiyo mara mbili au tatu kwa mwezi, lakini sio zaidi ya mara moja kwa wiki.

Takriban asilimia 25 waliripoti kupanda kwa hisia za tendo la ndoa ikilinganishwa na zaidi ya asilimia 17 miongoni mwa wanawake.

Athari zilizorekodiwa wakati wa majaribio hayo, ni pamoja na kichwa kuuma, kichefuchefu, kuwa na madoa doa mekundu usoni na katika ngozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,315FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles