26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Dar kuendelea kukosa maji

Sharif 01Na Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

WIZARA ya Maji imesema jiji la Dar es Salaam litaendelea kukabiliwa na uhaba wa maji, kutokana na uboreshwaji wa miundombinu yake kushindwa kukamilika kwa wakati.

Hadi sasa mradi mkubwa wa maji kwa ajili ya jiji hilo umefikia wastani wa asilimia 68.

Akitoa taarifa ya miradi inayotekelezwa na kuboresha huduma ya majisafi na majitaka katika jiji hilo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Maji na Mifugo, Athumani Sharifu, alisema jiji la Dar es Salaam linakabiliwa na changamoto ya maji kwa kiwango kikubwa.

Alisema changamoto hizo zinasababishwa na miundombinu ya barabara, nyaya za mawasiliano, nguzo za umeme, nyumba za watu pamoja na kesi zilizofunguliwa mahakamani pamoja na kuchelewa kulipa madeni ya wakandarasi ambayo yamefikia Sh bilioni 27.

“Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Marekani la Millenium Challenge Co-operation (MCC) wamekamilisha upanuzi wa chanzo cha maji cha Ruvu Chini  na upanuzi wa mtandao wa kusafisha maji” alisema.

Aliendelea kusema kuwa ujenzi wa bomba kuu la kusafirisha maji kutoka Ruvu Chini kuelekea Matenki ya Chuo Kikuu cha Ardhi kazi ya kulaza bomba lenye kipenyo cha meta 1.8 na urefu wa kilomita55.92 imeanza.

Alisema kazi hiyo ilianza Mei 2013 inaendelea ambapo hadi kufikia Juni mwaka huu, jumla ya kilomita 52.7 kati ya kilomita 55.92 sawa na asilimia 94.25 za bomba zimelazwa.

Pia alisema Serikali kwa kutumia mkopo nafuu wa Serikali ya India inatekeleza upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu ambapo ulazaji wa bomba kutoka Mlandizi hadi Kimara pamoja na ujenzi wa Tenki jipya Kibamba na kukarabati matenki ya maji kimara unaendelea.

Kukamilika kwa mtambo wa Ruvu Juu utaongeza uwezo wa kuzalisha maji kutoka lita milioni 82 kwa siku hadi kufikia lita milioni 196 kwa siku na kazi hii itagharimu dola za kimarekani milioni  39 ambazo ni sawa na Sh bilioni   70.2 za kitanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles