25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Jela miaka saba kwa kukamatwa na shanga za meno ya Tembo

FARAJA MASINDE NA GODFREY MBANILE (GPC), DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, imemhukumu kwenda jela miaka saba sambamba na kulipa faini ya Sh milioni 20, Feng Quan (38), raia wa China, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na goroli 767 za shanga zilizotengenezwa kwa meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 5.8 ambayo ni nyara za serikali.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, John Msafiri, baada ya mtuhumiwa kukutwa na hatia ya kutumia nyara hizo zenye uzito wa kilo 6.10 ambazo ni mali ya Serikali.

“Mahakama inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka saba jela sambamba na kulipa faini ya Sh milioni 20, ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo za kutumia nyara za serikali bila kuwa na kibali,” alisema Hakimu Msafiri.

Upande wa mashtaka ambao ni serikali, ulikuwa na mashahidi watano ambao wote waliithibitishia mahakama hiyo juu ya mtuhumiwa kukutwa na nyara hizo kinyume cha sheria.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Erik Shija, alidai kuwa mahakama haikuwa na kumbukumbu ya makosa ya nyuma dhidi ya mshtakiwa na hivyo kuiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Hata hivyo mtuhumiwa hakufika mahakamani hapo baada ya kuruka dhamana, jambo ambalo liliilazimu mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo upande mmoja kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 266, ambapo mtuhumiwa ataanza kutumikia kifungo chake mara tu baada ya kukamatwa.

Katika maelezo ya awali mtuhumiwa alidaiwa kutenda kosa hilo Desemba 22 mwaka 2013 eneo la Uwanja wa Ndege (Airport) akiwa na shanga hizo zenye thamni ya Sh milioni 5.8 zilizotengenezwa kwa meno ya tembo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles