24 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Dangote Cement yawa tishio Afrika Mashariki

dangoteNa Mwandishi Wetu

Kiwanda cha saruji cha Dangote kimefanikiwa kuhimili ushindani wa biashara ya Saruji Afrika Mashariki na kuongoza soko kwa muda mchache tokea uanze shughuli zake na kuwa gumzo katika eneo hili kwa kuwashinda vigogo wa biashara hiyo.

Miezi miwili baada ya kuanza Dangote imeweza kushika soko la Tanzania kwa asilimia 22 na kuweza kuuza saruji yake Kenya kutokana na bei yake shindani nahivyo kusababisha kampuni alizozikuta kujipanga upya kukabiliana na kampuni hiyo.

Mmiliki wa kampuni hiyo ambaye ni tajiri mkubwa katika Afrika, Aliko Dangote ana falsafa kuu ya kuuza uwingi kwa bei rahisi na hivyo kuwashinda wengi wanaouza kidogo kwa bei ya juu. Dangote ilifungua kiwanda chake mwezi Juni mwaka huu na pamoja na deni la kulipa la dola milioni 600 la ujenzi wakiwanda ameweza kuvuruga soko kwa kuuza bidhaa zake bei nafuu na vilkevile kuweza kupeleka na kuuza saruji nchi za nje na haswa Kenya amabayo ina miradi mingi ya ujenzi mkubwa.

Uingiaji Dangote Tanzania umemstua Tanzania Portland Cement (TPCC) ambaye alikuwa anaongoza kwa biashara na uzalishaji Tanzania na sasa anashuhudis soko lake likimegwa kidogokidogo na Dangote ambayo inakadiriwa sasa kushika nafasi ya pili ikiwa na asilimia 25 ya soko la Tanzania.

Lafarge Holcim ya Ufaransa ni mzalishaji mkubwa wa saruji katika Afrika na anatawala soko la Afrika Mashariki akiwa anamiliki asilimia 27 ya soko Afrika Mashariki na Tororo Cement ya Uganda ni ya pili kwa kumiliki asilima 21 ya soko ikifuatiwa na Athi River Cement (ARM) ya Kenya kwa asilimia 17 na hivyo kupata hasara ya dola milioni 3.64 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu.

Inasemekana hasara hiyo imetokana na kuingia kwa Dangote Cement kwenye soko la Kenya na bei yake shindani na hupelekea wateja saruji yake mlangoni kwa gharama zake. Kutokana na tarifa ya Global Cement ushindani wa bidhaa ya saruji umeshamiri Afrika Mashariki yote na hivyo kufanya biashra hiyo kuwa ya kunyang’anyana sana na wanyonge karibu watafunga viwanda.

Ukiachia Tanzania kule Mtwara Dangote ina kiwanda kingine cha saruji Ethiopia ambacho kinauwezo wa tani milioni 1.6 kwa taarifa za Juni mwaka huu zikizidi zile za mwaka 2015 ambapo ilikuwa tani 922,000 wakati kama muda huhuo; wakati kile kiwanda cha Mtwara uwezo wake wa uzalishaji ni tani milioni tatu.
Dangote Cement inajipanga na ikiwa na dhamira ya kuing’oa Lafarge Holcim kinarani kama mzalishaji mkuu wa saruji Afrika.

Sio hivyo tu Dangote anampango kabambe wa kuanzisha kiwanda cha saruji nchini Kenya ikifikia mwaka 2019.
Kampuni ya Dangote saruji yake huuza dola 74 nchini Kenya na Tanzania dola 80 bei ambayo ni ndogo (rahisi) kwa asilimia 40 ukifafanisha na washindani wake na hivyo kupata kwake soko sio shida na hivyo kuua biashara za wengine ambao wanafanya biashara kimazoea na sio kiushindani.

Geeska Afrika imetoa Ripoti kuwa bei ya rejareja kwa mfuko wa saruji wa kilo 50 ni dola 4.70 nchini Kenya wakati Tanzania ni dola 4.50 na dola 6.90 nchini Ethiopia.
Mahitaji ya saruji yanakua

Kwa wakati huu saruji inahitajika sana Afrika Mashariki kutokana na miradi mikubwa inayoendelea ya miundombinu mbalimbali katika eneo hili ambayo inaonesha itabeba kwa safari ya mbele ya uchumi wa bara la Afrika.
Nchini Tanzania kuna miradi ya reli ya Kati kuwa ya SGR, bandari ya Mtwara, Upanuzi wa banadari ya Dar es Salaam na ile ya Bagamoyo, Ujenzi wa bomba la mafuta ghafi ya Uganda kwenda bandari ya Tanga, Mradi wa Mchuchuma na Liganga,Ujenzi wa Reli Makambako hadi Mtwara na LNG Plant Lindi, Kiwanda cha Mbolea Lindi na kile cha grafaiti cha Ruangwamkoa wa Lindi.

UPanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, barabara za juu Dares Salaam na mkiundombinu ya majitaka Dar ujenzi wa makao makuuu Dodoma.

Kenya kuna ujenzi wa Reli ya SGR kwenda Uganda hadi Rwanda, Mradi Lassmet, ujenzi Bandari ya Lamu na barabara kwenda South Sudan na maboresho ya njia za Nairobi kwa njia za juu (flyovers).
Uganda kuna ujenzi wa bomba la mafuta na miundombinu ya mafuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles