25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

DAKTARI BINGWA AELEZA MADHARA ZA CHOKLET KWA WAJAWAZITO

Na AVELINE KITOMARY

DAR ES SALAAM

DAKTARI Bingwa wa watoto kutoka Chuo kishiriki cha Sayansi ya Afya Muhimbili (MUHAS) Dk Fransis Furia ameeleza kiwango cha chai na kahawa ambacho kinatakiwa kutumiwa na mjamzito.

Dk Furia alisema kuwa kuna madhara makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni endapo mama atatumia kiwango kikubwa cha majani ya chai na kahawa.

Akizungumza katika mahojiano maalum na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam DK.Furia alisema kuna kiwango ambacho kinatakiwa kitumike ni mg 200 bila kuvuka.

“Kahawa ina cafen ambayo inaleta madhara kwa mjamzito na tafiti zionaonesha kuwa watu wanaotumia vinywaji vya cafen wanaweza kupoteza ujauzito kwa mimba kutoka ,wakapata watoto wanaozaliwa kabla ya miezi kutimia(njiti) na uzito pungufu.

Dk Furia alisema matumizi hayo pia yanaweza kusababisha mjamzito akapata shinikizo la damu

“Tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya vinywaji vyenye cafen kwa kiwango kikubwa zaidi ya mg 200 kwa siku ina kuwa na madhara na unaposema mg 200 kuna vinywaji tofauti zina cafen tofauti kikombe kimoja cha chai kina mg 75 za cafen,kikombe kimoja cha kahawa ile ambayo unachukua na kuweka yaani kahawa ya unga ile unayoweka kwenye kikombe cha maji ile ni mg 100.

“Lakini kuna zile kahawa ambazo zinawekwa kwenye filter ambayo ni kali ile kikombe kimoja kila mg 140 kwahiyo shirika la afya Duniani linashauri kina mama wajawazito watumie kiasi kidogo cha vinywaji vyenye cafen na tunaposema kiasi kidogo wasizidishe mg 200 kwa siku?”alisisitiza.

Alisema mama anatakiwa kunywa vikombe viwili kwa siku vya kahawa lakini cola ya kopo ina mg 40 za cafeni mama anayekunywa cola za kopo akinywa nne tayari amefikisha mg 200 hivyo akizidisha ni hatari.

“Tunawashauri kinamama wajawazito wakati huo wawe wanazingati kuwa hawatumii chai kwa kiasi kikubwa ,kahawa na choklet kwani hata coklet ina cafen pia hivyo matumizi ya choklet ni hatari.

” Hatuwezi kubaini kama mtoto akizaliwa njiti chanzo chake ni nini kwani kunasababu nyingi na mara nyingi hatufatiliii lakini kuna haja ya kudhibiti matumizi hayo,Wakinamama wanashauriwa kula vyakula bora ambavyo vitampa afya bora kwake na kwa mtoto,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles